Underrated musicians in Tanzania

Hapo kwa Barnaba nimekuelewa maana Barnaba pengine hana kile kinaitwa bahati maana yule ni mtunzi mzuri na pia ni muimbaji mzuri sana kuwai kutokea...Na ukitaka kuamini hayo uliza ni nyimbo gani amewatungia watu na zimefikishwa wapi? Watu wote alio watungia nyimbo wamepiga hela mfano Vannesa,Rubi,Peter msechu,Dyna Nyange,Shilole..Wote hao kila wimbo alo watungia zimekuwa hit kali.

Mwanzo nilidhani tatizo management na promo lakini I was wrong maana Barnaba alishakuwa chini ya THT ya Clouds na promo alipewa sana na kila media humpa support lakini wananchi hawampokei ipasavyo...
Kwakweli hadi leo sijawai pata jibu kwanini Barnaba hakui kimuziki?Nabaki kusema kuwa hana bahati jambo ambalo uwezi kulieleza au kulitolea ushahidi.

Ninachoweza kusema tuu ni kuwa Barnaba pole sana.
 
Anyoe rasta atakubalika [emoji3] [emoji3]
 
Rama Dee
Vitalis Maembe
 
One sjiui ana kimavi gani yule dogo,anajua kinoma lakini dah,
Ila Nick Mbishi is just wack!
 
Barnaba boy ni mzuri kwenye utunzi.
 
Barnaba kuna upande ambao yuko underrated na upande ambao yuko fairly-rated, upande ambao yuko underrated ni wa mashabiki, mapokeo ya kazi zake kwa mashabiki sio makubwa kihivyo ingawa sio madogo pia, ila kwa upande wa media zinampa promo za kutosha na sio clouds tu karibu media zote, na yuko well appreciated na wasanii wenzake as well as watangazaji nimekuwa nikiona wakimsifu mara kwa mara. Kwahiyo naweza sema kuna vitu wasanii wenzake & watangazaji wanaviona kwa Barnaba ambavyo mashabiki wengi wanashindwa kuviona. Kwa upande wangu namkubali Barnaba kwenye utunzi na uimbaji, ila ananiboaga jukwaani tu, ni miongoni mwa performers wabovu sana, hajui kuentertain awapo jukwaani, mimi huwa namkata maksi hapo tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi kuna wasanii naonaga hata wakitoaga nyimbo kali wanachukuliwa kawaida, yaani nobody care, na ni ngumu kuona mtu anawasifia, mfano Chege, Madee, Gnako, n.k sijui nao tuwaweke kundi hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…