Undetectable Untransmittable

Undetectable Untransmittable

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Ni kuhusu HIV, wengi huu ugonjwa umetuathiri kama sio sisi basi ndugu zetu wa karibu. ARV’s kwa kweli amekuwa mkombombozi na wengi wanaishi kwa miaka mingi tena wakiwa na afya njema.

Ukiwa Undetectable uwezo wa kumuambukiza mtu mwingine ni mdogo sana. Hii haimaanishi umfiche mchumba kuwa wewe ni mwathirika la hasha ila unaweza kumuekeza na kumtoa hofu kuwa hutamuambukiza.

Imefika mahala tuache kuwacheka waathirika kwani hakuna anaefahamu kesho yake. Kama ndugu yako wa karibu ameathirika mpe moyo wa kuendelea na tiba. Usiwe mnyonge Undetectable Untransmittable.
 
kuwa undetectable ndio kuwaje??
Mgonjwa anapotumia dawa na kufanikiwa kuondia viral load au virus vitembeavyo kwenye damu.

Haimaanishi kuwa amepona kwani akiacha kutumia dawa viral load inarudi.
 
Nahisi kama unaongea na mimi, huu ni uzi wako wa pili kuhusu ukimwi tangu nijiangushe uwanjani.

Nilipimwa HIV miezi miwili nyuma sikukutwa nao. Nimejiangusha uwanjani wiki mbili nyuma, lini niende kupimwa tena?
Namaanisha lini virusi vitaonekana?
 
Kwa miaka mingi tulizoea window period ya miezi mitatu. Sikuhizi kuna advance technology virus huonekana baada ya wiki mbili. Ulizia technology iliyopo kwenye clinic iliyokaribu nawe.
 
Kwa miaka mingi tulizoea window period ya miezi mitatu. Sikuhizi kuna advance technology virus huonekana baada ya wiki mbili. Ulizia technology iliyopo kwenye clinic iliyokaribu nawe.
Clinic niliyo karibu hapana. Wapi kuna hiyo technology kwa Dar es Salaam?
 
Ili mtu aweze kuwa undetectable ni mambo gani anatakiwa kuyafata katika mtindo wake wa maisha na ni vitu gani anatakiwa kuviepuka asivifanye ili afya yake iwe poa zaidi?
 
Back
Top Bottom