UNDP: In the long run, COVID19 will have significant risks to sectors in Tanzania especially tourism

UNDP: In the long run, COVID19 will have significant risks to sectors in Tanzania especially tourism

Hebu waambieni hao UNDP watuache....

Watu tumejifukiza na moshi wa Mwenge wa Uhuru miaka yote....


Wasilete upuuzi wao.
 
Kiazi mwingine huyu hapa🤦🏾‍♂️
Hujanielewa!! Nilikua namponda huyo jamaa kwamba hajaelewa andiko, kwa sababu limeandikwa “Kichaga”, nikimaanisha English! Niondolee ukiazi ndugu yangu!!
 
Nadhani, ili kutupa nasi moyo ikiwa pamoja na kuwajibu hao walotoa hiyo report, ungetusaidia basi na taarifa za idadi ya (hapa Tz) waliopimwa, waliokutwa na maambukizi,waliolazwa, vifo na waliopona, kwa mwezi april , may mpaka sasa; ingefaa kwa siku. Siye wengine hatujazipata muda sasa. Natanguliza shukurani kwako.
Unataka idadi ya corona ili iweje mbona hujauliza wagonjwa wa malaria ambayo ndiyo inaongoza kuua watz? Usikopi toka uzunguni wazungu ugonjwa wa corona ndiyo ugonjwa unaowasumbua.
 
Unataka idadi ya corona ili iweje mbona hujauliza wagonjwa wa malaria ambayo ndiyo inaongoza kuua watz? Usikopi toka uzunguni wazungu ugonjwa wa corona ndiyo ugonjwa unaowasumbua.
Pole mada mbele yetu haikuwa malaria. Waonekana hauna data zozote za corona, ila una hoja hewa za kutosha.
 
Tumewazoea washasema mpaka Mei tugekuwa tumekufa 10,000 lakini tunadunda. Wapo wafanyakazi huko UNDP wanaandika ripoti ili kuwafurahisha wazungu ili walete pesa. Wapo wengi tu wanaopika data sisi wengine tumefanyakazi huko tunaujua mchezo.
Labda ulifanya kazi ya kufagia vyoo maana hata ukijua Kisukuma tu unaweza fagia. Lugha ya report hiyo hata wenye zile PhD toka kule hawaoni ndani.
 
Hii assessment ni kwa nchi zote zenye UN. Niko Ghana. UNDP pia wametoa report kama hiyo. Haya ni maagizo ya SG Guterres. Usijijengee maadui ambao hawapo. Usiwe paranoid.
Kumbe nchi zote UN,mbona imeletwa kishabiki as if reports inahusu Tanzania tu?
 
Watahangaika sana na Tanzania ila hawataweza

Baba wa Taifa alitufundisha jinsi ya kuishi na maadui wanaojifanya marafiki
Mabeberu wamesubiri miili/maiti zizagae barabarani hadi wamechoka!! Sasa wameachana na miili kuzagaa wamekuja na "unabii" mwingine!! Wanadai athari za muda mrefu kwenye utalii! Cha kujiuliza ni:
1. Je hizo athari ni kwa Tanzania tu? kwa sababu tulikataa upuuzi wa lockdown?
2. Je nchi zingine hazitaathirika kwa kuwa zilifanya lockdown?
Ukweli ni kwamba nchi zote zitaathirika lakini athari kwa nchi zingine zilizofanya lockdown ni kubwa zaidi kuliko sisi! Hilo wanalijua lakini hawalisemi! Wivu unawauma!
 
Wanaotaka data za corona Tanzania ni sawa na kutafuta data za meli jangwani! Tanzania hatuna COVID 19, Mungu ameiondoa!! Wanaotaka data za corona waende Kenya au Marekani! Huko ndiko kuna COVID 19
 
Back
Top Bottom