Unene na uzito umeongezeka baada ya kuanza mazoezi, mgongo na kiuno maumivu makali yanaendelea.

Unene na uzito umeongezeka baada ya kuanza mazoezi, mgongo na kiuno maumivu makali yanaendelea.

mjasiriamali mdogo

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2013
Posts
258
Reaction score
110
Kabla sijaanza mazoezi nilikuwa na kilo 84 lakini cha kushangaza jana nimepima nimekuwa na kilo 85.5. Huwa nazunguka uwanja mara 15 na mazoezi ya viungo na kucheza mpira kila asubuhi lakni unene na uzito vinaongezeka.

Tatizo lingne maumivu makali ya mgongo na kiuno ilinifanya mpaka kuja Dar Muhimbili kwa vipimo lakini MRI na X-Ray hawakuona kitu. Mgongo na kiuno jamani vinanisumbua sana, nikinywa dawa maumivu hupotea lakini baada ya wiki 1 maumivu hurudi tena. USHAURI WA TIBA NA MAWAZO.
 
Punguza uzito kilo 84 ni sheeda jitahidi ufikishe kilo 65,ukifanya mazoezi na ukaendelea kula vile vile lazima utafutuka tu.
 
Pole sana mkuu, kwa ushauri wangu ni vyema mtu unapoanza mazoezi kwa lengo la kupunguza mwili basi jitahidi na kuangalia upande wa chakula, namaanisha usile chakula kingi kizidi mahitaji ya mwili, usile vyakula vya mafuta sana, usile vyakula vilivyotayarishwa viwandani (junky food).
Kuna wakati mtu anafanya mazoezi kwa lengo la kupunguza mwili asubuhi sana, akitoka mazoezin anakula msosi wa kufa mtu tena wenye mafuta sana kama vile supu na chapati nyingi, hapa naamini ni sawa na kupunguza uzito 1kg then kila siku unafanya juhudi za kuongeza 0.9kg mwisho wa siku unajikuta mafanikio yako ni 0.001%
 
Back
Top Bottom