Pole sana mkuu, kwa ushauri wangu ni vyema mtu unapoanza mazoezi kwa lengo la kupunguza mwili basi jitahidi na kuangalia upande wa chakula, namaanisha usile chakula kingi kizidi mahitaji ya mwili, usile vyakula vya mafuta sana, usile vyakula vilivyotayarishwa viwandani (junky food).
Kuna wakati mtu anafanya mazoezi kwa lengo la kupunguza mwili asubuhi sana, akitoka mazoezin anakula msosi wa kufa mtu tena wenye mafuta sana kama vile supu na chapati nyingi, hapa naamini ni sawa na kupunguza uzito 1kg then kila siku unafanya juhudi za kuongeza 0.9kg mwisho wa siku unajikuta mafanikio yako ni 0.001%