Unene wa mke wangu unamuweka matatani

Unene wa mke wangu unamuweka matatani

chai chungu hii, kama haoni hizi comments, ze big hebu kwanza jibu maswali, hii chai au gahawa, ukiwa muongo uwe na kumbukumbu
Sio kila ninacho andika kinanihusu direct kuna watu wana matatizo na hawana simu . JE HAWARUHUSIWI KUOMBA USHAURI KUPITIA KWA MTU KAMA MIMI?
 
Hii inaweza ikawa ni sababu kubwa ya hili. Sasa walipokaa na mumewe kuongea kuhusu unene wake kwanini hakuliongea hili labda hali ya nyumbani/kazini inampa stress katika maisha yake? Pia walipoenda kumuona Dr angeweza kabisa kusema chochote kile kwa Dr ambacho kingeweza kumpa fununu Dr kwamba huyu mdada ana stress.

Mkeo ana stress...
 
Sio kila ninacho andika kinanihusu direct kuna watu wana matatizo na hawana simu . JE HAWARUHUSIWI KUOMBA USHAURI KUPITIA KWA MTU KAMA MIMI?
kwa hiyo hapo wewe ni yupi? mwenye mke kibonge au anayeshindwa kuishi na mwanamke, kwanini usiwe wazi ili kuondoa hizi inconvinience.
 
Haraka haraka nahis mkeo anatumia njia za uzazi kwa siri...yaweza kuwa vidonge au sindano..wamama weng hufanya siri hili jambo..mana si kwa unene huo wa ghafla

Hapana, tatizo ni ulaji iliyopitiliza mipaka - kisaikolojia naona anahisi mumewe hampendi vya kutosha, wanawake wengine wana mawazo ya ajabu sana - kwa hiyo anahamishia hasira zake katika kula bila mpangilio, watu wengine wanaweza kufikiri natania lakini ukweli ndio huo - mumewe ajaribu kuangalia tatizo hilo lilianza lini na mahusiano yao yalikuwa katika hali gani wakati ananza kula kula ovyo na kumjibu jibu kimkato mkato.
 
Mkeo ana stress...
Kuna mtu nilimwambia kunenepa sana ni stress akabisha saana akisema hilo lina apply Ulaya...
Sio siri hata mimi nikiwa na stress natafuta cake...
Tukirudi kwenye mada huyu wife ni kiboko...
Anamfokea hadi daktari...
Sasa hapo utatumia njia gani kumshawishi aache kula hovyo...

Maana njia rahisi ilikuwa umtumie doctor amdanganye kuwa anakaribiea kufa achangue kula au kuishi...
Sasa mtukana madaktari utamfanyeje...?!

Mkataa pema huyu...
Na ukishafika kilo 110 kuzitoa kunataka moyo si kuburuzwa...

Au kwao ni vibonge...maana mi hata nileje 110 haziwezi kufika...
Angekuwa 44 ndio mwili wake wa asili asingefika hiyo 110...hata aleje angecheza sana sana na 60s...huyo labda ana unene wa ukoo ambao unahitaji descipline ya hali ya juu kuukwepa...ukiiingia kutoka hadi mazoezi ya kijeshi...

Na usipoangalia atakuharibia na watoto...watoto wa mama mlaji nao lazima wawe vibonge
 
Mtafutie make mwenza na yes MPE 33% au kamuone Mwaka dokta
 
Nilifanikiwa kupata mwenza wa maisha (kuoa) mnamo mwaka 2006 kipindi ninaoa mimi nilikua na uzani wa kilo 50 na wife alikua na kilo 42 maisha yalisonga tukapata mtoto wakwanza. Wife alijifungua normal kabisa na tukalea mtoto wetu wa kwanza wife alikua na kilo 44 mpaka mwanetu anafikisha umri wa miaka mitatu mwaka 2009. Tukafanikiwa kupata mtoto wa pili ambae Mungu si athumani wife alijofungua salama pia na mpaka mwanetu anafikisha miaka mitatu wife alikua na kilo zile zile 44.

Hatujawahi kutumia njia yeyote ya uzazi wa mpango ila mnamo mwaka 2014 wife alianza kunenepa katika kipindi cha mwaka mmoja alitoka kilo 44 mpaka 76. Nilijitahidi kumshawishi japo kwa njia ambayo isinge mkwaza kua tuwe tunakimbia kimbia jioni wife akisikia swala la mazoezi anakua mkali nitanuniwa hata wiki tatu haongei yeye ni ku deal na watoto tu.

Ilipofika mwaka jana mwishoni wife alifikia kilo 95 kuna kipindi alikuwa anappata dalili za pressure tukaenda hospitali daktari alimshauri apunguze weight lakini alimgombeza daktari kama mtoto mdogo kua amuache yeye ni mtu mzima kama kumtibu ameshindwa aseme. Sikuwa na jinsi zaidi ya kua mpole na kupewa baadhi ya vidonge na kurudi nyumbani.

Mwezi uliopita wife amefika kilo 110 ambazo zinazidi kumuweka katika hatari yakupata magonjwa mengine ya hatari zaidi. Ameanza kukoroma kwa sauti kubwa sana usiku na akilala hataki umuamshe hata kama kuna kitu chochote kile amekua mkali sana na hata haki ya ndoa anasema anachoka sana skuizi ananipiga kalenda. Unene wa wife umekua ukinipa uoga na kumuonea mke wangu huruma sana hasa nikiona anapokua akilalamika miguu inamuuma.

Kuna siku nilijaribu kumwambia miguu inakuuma kwasababu ameongezeka uzito katika kipindi kifupi mno, hili lilizua ugomvi mpaka tukaenda kusuluhisha kwa wazazi baada ya miezi miwili ya kuvutiwa mdomo na kukosa amani ndani ya nyumba kwa kumshauri wife jambo la busara tu.

Kwa sasa nina kilo 54 wife anachezea 110 ninaomba ushauri nifanyeje wife anielewe na aweze japo kufanya mazoezi amekua kibonge sana na anapata matatizo ambayo yananiogopesha naweza kumpoteza mama watoto. Nilishawahi kujaribu kumshauri tujiunge kwa pamoja gym hilo ndilo lilizua maneno kuwa ninafuata wanawake huko gym namshangaa wife japo ni msomi ana masters yake ila haoni umuhimu wa afya yake.

Kitu kinachomfanya wife awe hivi ni kula kupita kiasi na kupenda sana vitu vya wanga kuna siku kulikua na birthday ya mwanetu alikula keki ya kilo tatu na ile sukari ya juu yote baada yakuwakatia watoto. Anaweza kutoka kazini akapita mahali akala hata kilo mbili za kitimoto, kuna siku nilimfuma anakula kitimoto bar kwa makadirio kilikua kama kilo 2 nikajaribu kudadisi nikagundua huwa ana desturi yakupita pale kila siku na ameweka oda kabisa na akifika nyumbani pia anafanya majukumu yake vizuri ikiwa ni pamoja na kuwapikia watoto na hula tena mara yapili na kulala akimaliza tu kula.

Ninaombeni ushauri ndugu zangu nifanyeje kunusuru afya ya mke wangu.
we na mkeo wote mna matatizo. mtu una 54kg unajiita ze big???
 
Sasa mtu kashafikia hatua ya kula kilo 2 za nyama hakuna la zaidi ya kuandaa mazishi maana tiba haitaki.
 
Natamani awe mke wangu, mimi na matipwa tipwa ni kama maji na samaki, tai na shati, sindano na uzi.
Hapo kuwa mpole, be smart to her, ongea naye kiromantic coz yawezekana unaongea naye kimwanaume gubu. Hana furaha na wewe coz anaona unamsema kuhusu mwili wake wala sio kumsaidia sasa penzi atakupa kwa raha gani?
 
Back
Top Bottom