UNESCO: Wenyeji wa Ngorongoro Wahame. Wafanyakazi wa NCAA na Mahoteli waishi nje ya Hifadhi

UNESCO: Wenyeji wa Ngorongoro Wahame. Wafanyakazi wa NCAA na Mahoteli waishi nje ya Hifadhi

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
UNESCO: Wenyeji wa Ngorongoro Wahame. Wafanyakazi wa NCAA na Mahoteli waishi nje ya Hifadhi

Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro si eneo ambalo ni Hifadhi ya Taifa na vile eneo hili la Ngorongoro halipo chini ya shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na badala yake ni shirika huru kama jinsi ilivyo TANAPA likijitegemea kazi na majukumu ya TANAPA na Ngorongoro yanafanana katika kuhifadhi viumbe hai na makazi yake kuwa endelevu kwa ajili ya vizazi vilivyopo na vijavyo.

Lakini kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ni eneo ambalo ni hifadhi mseto ambapo kuna viumbe hai aina tatu vikiishi kwa pamoja ambavyo ni watu ambao zaidi ni jamii ya kabira la wamaasai, mifugo yao kama kondoo, mbuzi na ngo’mbe na wanyamapori.

HISTORIA YAKE:
Sababu ya msingi iliyopelekea kuanzishwa kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ni ukweli wa mambo ya kwamba jamii ya kabila la maasai ilikuwa likiishi katika eneo la Serengeti na Ngorongoro kwa miaka mingi pamoja na wanyamapori.

Wamaasai ni jamii ya nilotiki ambao asili yao ni kusini mwa Sudan na ni jamii ya wafugaji kiasili. Kwa kuwa jamii ya wamaasai ilikuwa ikiishi ndani ya maeneo haya ya uhifadhi pasipo utaratibu maalumu na mwongozo jamii hii ya kabila la wamaasai ilikuwa katika janga kubwa la wanyamapori kama vile magonjwa maambukizo ya wanyamapori na majanga mengineyo.

Hivyo basi serikali ya wakoloni Waingereza wakati wa kipindi hicho iliamua kuanzisha maeneo mawili tofauti ya uhifadhi eneo moja la uhifadhi litumike maalum kwaajili ya uhifadhi wanyamapori pekee ambayo ndio Serengeti ya leo hii na vile vile eneo jingine la uhifadhi llitumike kama Hifadhi mseto ambapo wamaasai wataishi kwa pamoja yaani (Conservation). Hatimaye wamaasai wote waliokuwa wakiishi Serengeti ya wakati wa kipindi kile wakahamishiwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ya leo hii.

Vilevile malengo mengine yalikuwa ni katika kulinda maslahi ya jamii kabila la wamaasai ambao wameishi na wanyamapori pasipo uharibifu wowote ule kwa miaka mingi jamii ya kabila la wamaasai wanachukuliwa kuwa ni wahifadhi asili kwa sababu ya kuishi na wanyamapori kwa muda mrefu kihistoria.

Ikumbukwe naieleweke hapa ya kwamba hifadhi za Taifa zote zilipo chini ya shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) pamoja na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro uanzishwaji wake ulikuwa ni mwaka 1959.

Aprili 17, 2018 ilitambuliwa na Umoja wa Matyaifa kupitia shirika lake la Elimu Sayansi na Utamaduni (Unesco) kuwa hifadhi jiolojia ya Ngorongoro Lengai hivyo kuingizwa kwenye mtandao wa hifadhi zenye hadhi hii duniani. Kijiografia inapatikana mkoani Arusha.

Eneo hilo linajumuisha Bonde la Ngorongoro (Ngorongoro Crater), Engaruka, Selela, Engaresero, bonde la Empakai, mlima Oldoinyo Lengai mlima pekee Tanzania ambao volkani yake bado ni hai, Bonde la Oldupai (Oldivai) sehemu ambayo ni chimbuko la historia ya binadamu.

MIVUTANO NA SULUHISHO
IMG_20220217_070159_281.jpg

HOJA ZA WENYEJI

*Vibali vya kujenga nyumba za kudumu ndani ya hifadhi

*Wanahitaji faida Zaidi kutokana na Mapato ya Utalii

*Hati Miliki ya Ardhi ndani ya NCA

*Waruhusiwe kulima ndani ya hifadhi

*Wanahitaji kujenga huduma za Kijamii ndani ya Hifadhi

HOJA ZA JAMII

*Wanahitaji marisho katika maeneo yayokatazwa kama Kreta, Northern Highland Forest Reserve (NHFR), eneo oevu la Ndutu)

*Wanahitaji kushirikishwa katika maswala yanayohusu Maamuzi ndani ya Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA)

*Fidia ya Mifugo inayoliwa na Wanyamapori (Compensation for livestock depredation and Human attacks)

*Mipaka Mipya imepunguza ukubwa wa eneo la Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA), hivyo jamii inaomba maeneo yaliyochukuliwa yarudishwe

USHAURI WA UNESCO

Unesco kwa Ujumla wake imeshauri yafuatayo:

*Yafanyike Mapitio ya Mfumo wa Matumizi Mseto ya ardhi ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro ambao kwa sasa umebainika kushindwa kufanya kazi ipasavyo

*Kuhamasisha uhamaji wa wenyeji kutoka eneo la hifadhi kwa kutoa Motisha kwa wenyeji ili waweze kuhama. Aidha UNESCO inashauri kuhamisha Wafanyakazi wa Taasisi ya Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) na Wafanyakazi wa Mahoteli ili waishi nje ya eneo la Hifadhi
 
Great thread hapa kuna cha kuongea sasa pamoja na kuwepo zile blah blah nyingine.

Kama UNESCO wametoa info's basi something going to move although nashangaa maasai walitolewa mkoani Mara na kuletwa Arusha ila leo hawataki kuondoka tena, yaani teknolojia ina wasaidia sana nowadays.
 
USHAURI WA UNESCO

*Kuhamasisha uhamaji wa wenyeji kutoka eneo la hifadhi kwa kutoa Motisha kwa wenyeji ili waweze kuhama. Aidha UNESCO inashauri kuhamisha Wafanyakazi wa Taasisi ya Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) na Wafanyakazi wa Mahoteli ili waishi nje ya eneo la Hifadhi
Win win situation.
Naam, muafaka huo utakuwa ni wa faida kubwa zaidi kwa pande zote.
Tuupigie chapuo!
 
NCAA waliharibu wenyewe kwa kutengeneza kile kinachoitwa kwa kiingereza escalation of situation.
Kulikuwa na haja gani ya kuwatumia kina Kitenge na Balile kuidhalilisha jamii?
Kama hiyo mamlaka ina watu walioenda shule na kupata exposure kweli, kulikuwa na sababu ya kuwatweza wamasai hadi wamaasai wote popote walipo wamekasirika na kupata hasira?
Je, hawajui hali ya vijiji katika mikoa mingine kama Kigoma, Rukwa, Katavi, Songwe, Mtwara, Singida, Dodoma, Mara, Simiyu, Mbeya, Shinyanga, Manyara nk kwamba ni zaidi ya pale NCA na hawaishi na wanyama?
Kwanini waidhalilishe jamii bila kufanya utafiti?
Kulikuwa na haraka gani?
Walishindwa kusubiria michakato ya serikali yenye kuzingatia maslahi ya pande zote kama hii inayofanywa na waziri mkuu Kassim Majaliwa?
Kulikuwa sababu gani ya kutapanya fedha za umma kutengeneza chuki, dharu, dhalili na hofu kwa wananchi maskini kwa kutumia fedha mlizochuma kutoka katika ardhi ya mababu zao hata kama ninyi mnajua ni ya Rais?
 
HOJA ZA WENYEJI

*Vibali vya kujenga nyumba za kudumu ndani ya hifadhi

*Wanahitaji faida Zaidi kutokana na Mapato ya Utalii

*Hati Miliki ya Ardhi ndani ya NCA

*Waruhusiwe kulima ndani ya hifadhi

*Wanahitaji kujenga huduma za Kijamii ndani ya Hifadhi
Duh Hawa wenyeji ndio kuna msemo wa lugha ya kigeni unaosema To have your Cake and Eat it too....

Yaani wapate faida kutokana na utalii wakati wanaendelea na shughuli zinazohatarisha huo Utalii....
 
Idadi ya masai ikizidi kuongezeka Ngorongoro mwisho wa siku wao na mifugo yao watageuzwa kitoweo cha Simba.
 
Wahamishiwe uraiani jamani wamasai wameshakuwa kama wanyama huko polini,wasaidiwe waletwe huku wachangamane na binadamu badala ya wanyama
 
Back
Top Bottom