Ukitaka kujua IQ zetu nenda kwenye daladala angalia jinsi watu watakavyojipanga kusimama ili wakae vzuri au wasimame vzuri,kuna wengine hata kusimama vzuri wanashindwa maana IQ yake ndo imefikia kikomo,mwenye IQ ndefu ataona tatizo na kumwambia simama hivi au shika hapa usimame vizuri,lingine upangaji wa mizigo ndani ya daladala,utakuta mtu anaweka mzigo namna ambayo ni kero kwa wengine na hao wengine wanamgombeza huyo alitua mzigo wake.
Nakupa mfano; kuna siku nilipanda daladala la Posta-Mwenge,ndani ya daladala kulikuwa na jamaa alivuja sana majasho,basi alichofanya ni kuvua tshrt lake ili kupunguza joto ndani ya daladala hapo!! sasa wengine wakaona siyo fair kuvua shati ndani ya daladala kuna jamaa mwingine alimwambia huyo aliyevua utavuaje shati ndani ya gari na hata sisi tunavuja majasho kama wewe lkn hatuvui,jibu alilotoa huyu jamaa alitamka maneno haya;ninyi wapumbavu kaeni kimya. Hapo IQ ya aliyevua shati ni ndogo hii ina maana katika mazingira yoyote anaweza kufanya lolote la kipumbavu!
The same to this mada kwamba wanaume ambao ni Unfaithful yawezekana kuwa na IQ ndogo lkn si wote hata wenye IQ kubwa wanaweza kufanya haya ila mara chache!