Ungana na mimi kwenye kundi la climate change activist tukalale barabarani

Ungana na mimi kwenye kundi la climate change activist tukalale barabarani

Maghayo

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2014
Posts
20,307
Reaction score
47,210
Mzuka Wanajamvi!

Tusipochukua hatua leo na sasa hivi vizazi vijavyo havitatusamehe kabisa.

Amkeni sasa hivi na muungane na mimi leo asubuhi kwenye kundi letu la climate change activists la just stop oil na extinction rebellion.

Bila uwoga tukalale na kukakaa barabarani kuelekea magogoni, Samora avenue, mwaikibaki, Sam Nujoma, bibi titi, azikiwe.

Pia tujigundishe daraja la Tanzanite, kijitonyama. Na bagamoyo road lugalo.

Tuwaunge mkono wanaharakati wenzetu huko ulaya wanavyofanya.

Tusiogope hivi ni vita. Hamuoni sasa hivi ukame. Dar mji mkubwa hauna maji. Hakuna umeme. Watu wanaoga na kunywa maji ya jumvi gizani.

Hii yote ni kwa ajili ya tabia nchi. Na shughuli za binadamu zisizofaa.

Majuzi Pakistan mafuriko. Ukame kila Mahali.

Tusipochukua hatua sasa hivi tutawaweka vizazi vyetu vijavyo katika wakati mgumu.

Wote kwa pamoja tukutane tujilaze na tukae barabarani. Hii italeta mwamko chanya na kupanua wigo mpana kupigana na kudhibiti uaribifu wa mazingira .
Screenshot_20221031-033520.jpg
Screenshot_20221031-033531.jpg
Screenshot_20221031-033541.jpg
 
Hii dunia kwisha ozone layer imeisha toboka vibaya ata ku -repair ni almost impossible subir kufa tu
 
Sasa mkuu si tukapande miti na kuacha kuharibu vyanzo vya maji?
Tukalale barabarani ili iweje?
Ndo njia mpya ya maandamano sasa hivi duniani dhid ya climate change
 
Kwani hakuna njia nyingine isipokuwa kulala barabarani. Hapo ni kutafuta shari
 
Ndo njia mpya ya maandamano sasa hivi duniani dhid ya climate change
Kwamba tukiandamana ndo mabadiliko yatatokea yenyewe kimiujiza? Tuandamane kushinikiza nini?
 
Unawajua policcm? Utapgwa mpaka uchakae. Kama wewe ni mwanamazingira tupe maneno hapa hapa.
 
Kwamba tukiandamana ndo mabadiliko yatatokea yenyewe kimiujiza? Tuandamane kushinikiza nini?
Yani tutalala tu na kukaa barabarani. Tena tutajinatisha na kujigandisha na superglue. Hang'oki mutu hata kwa virungu. Tumechoka na tumeamua liwalo na liwe. Kupanda miti imeubiriwa miaka nenda rudi lakini wapiii. Dawa ni iyo tuu hadi kieleweke.
 
Unawajua policcm? Utapgwa mpaka uchakae. Kama wewe ni mwanamazingira tupe maneno hapa hapa.
Tuko tayari kufa na kupigwa kutetea mustakabali wa vizazi vijavyo. Hatutaki tena vizazi vyetu vipotee kama dinasours
 
Yani tutalala tu na kukaa barabarani. Tena tutajinatisha na kujigandisha na superglue. Hang'oki mutu hata kwa virungu. Tumechoka na tumeamua liwalo na liwe. Kupanda miti imeubiriwa miaka nenda rudi lakini wapiii. Dawa ni iyo tuu hadi kieleweke.
Kwa kweli hilo utafanya mwenyewe, na jua lote hili nikajianike kwenye lami?

Wa kuleta mabadiliko ni sisi wenyewe..
Kama kupanda miti imeshindikana unadhani kuwakusanya watu mkalale barabarani inawezekana?
 
Kwani hakuna njia nyingine isipokuwa kulala barabarani. Hapo ni kutafuta shari
Njia nyingine nyingi zimetumika lakini wapi. Kwa iyo hii njia ya kulala na kukaa barabarani hasa rush hours Will be a waking up call na watu kutochukulia kimzaha mabadiliko ya tabia nchi. Na hii ikishindikana basi hatuna jinsi ni kunya hadharani tu barabarani.
 
Hayo maandamano yataondoa ukame siku hiyo
Hayataondoa siku iyo. Ila itasaidia na kuhamasisha. Kumbuka tunatendea haki vizazi vijavyo hali ya tabia nchi inatisha. Na hatutaishia hapo tutaendekea kwa kuvamia mabucha ya nyama na kuwakataza waache kuuza nyama. Ni wakati sasa hivi watu wajifunze kutokula nyama nakuwaonea huruma viumbe vingine.
 
😄😄😄
Mkuu hili siyo swala la kuchekea chekea hapa. Jiulize joto kali linavyosababisha vifo vingi. Tumehubiri wee upandaji wa miti wapiii. Watu sasa hivi wanatakiwa watembee kwa miguu au baiskeli. Ishu ya carbon emissions hairidhishi.

Jest imejin sasa hivi magari yaliopo barabarani ulimwenguni kote ni billion 2. Hii ni hatariiii kabisa kwenye tabia nchi.

Tunakaribisha uwepo wa magari ya umeme lakini ni machache na ghali. Tesla yenyewe tu ina magari million 3 ni kidogo
 
Tukutane Lugalo mkuu,ila wewe uwe mstari wa mbele kabisa na Bendera mkononi ukituongoza njia.

😅😅
Niko tayari. Nashukuru kwa kuniunga mkono. Wenzetu huko uingereza wametungiwa majina ya ajabu ajabu sijui eco Zealots sijui Eco idiots lakini historia itatukumbuka.
 
Hayataondoa siku iyo. Ila itasaidia na kuhamasisha. Kumbuka tunatendea haki vizazi vijavyo hali ya tabia nchi inatisha. Na hatutaishia hapo tutaendekea kwa kuvamia mabucha ya nyama na kuwakataza waache kuuza nyama. Ni wakati sasa hivi watu wajifunze kutokula nyama nakuwaonea huruma viumbe vingine.
Hili la kuacha kula nyama ushindwe na ulegee
 
Yeeee mkuu issue nzuri mno,Nami nimeachiwa nchi nzuri ningependa kizazi changu kijacho nacho kifaidi mazingira mazuri, bila shaka umesoma majibu ya dot. Com, kizazi cha kulalama kwenye social networks tu, kuna uzi muda huu humu kuwa watanzania wanapokua wanakabiliwa na matatizo makubwa mno, matatizo hayo yanawafanya wawe uji zaidi, sasa wanalalama kuhusu upungufu wa maji na wengine wanaomba ratiba ya mgao wa maji!
 
Back
Top Bottom