Ungefanyeje ili kurejesha amani nchini Congo DRC?

Ungefanyeje ili kurejesha amani nchini Congo DRC?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Kama ungelikuwa Rais wa Congo DRC, ungeweza kuifanya hiyo nchi kuwa na amani?

Naamini suluhisho la Congo DRC lipo kwa Wacongoman wenyewe! Lakini hilo wataweza kulifikia kupitia viongozi wao, kama wasemavyo "wahenga", "Everything rises and falls under the leadership"

Ingelikuwa wewe ndiye Rais, ungelifanyeje ili nchi yako ya Congo DRC iwe na amani ya kudumu?
 
Amani haipatikani ila Kwa UPANGA TU. ( Peace through strength).

Ondoa Majeshi ya KIMATAIFA huko... Ruhusu Mchina na Mrusi wakusaidie.

Ingiza Majeshi ya Nchi Rafiki , Jiimarishe Kisilaha, Kifedha .

Fanya Counteroffensive ya Nguvu , Piga piga mpaka uingie Rwanda, endelea kupiga tu Kwa Kila atakayeingia 18 awe ni Uganda muunganishe kwenye kichapo.

Siku Congo atafanikiwa kumpa Maumivu Mnyarwanda, mbona atakua mezani tu.

Shida Moja itakayobaki ni RC .
 
1:-Hakuna amani kongo bila Rwanda na Uganda dhaifu, so only way to peace in Congo, ni kuvamia Rwanda na kuishinda kabisa, na hapo wajiandae na Uganda make hawawezi kubali Swahiba wake achapike wapo.

2:- Usaliti usaliti usaliti, huu unaiua Congo, jeshi la ndani ya Congo kamwe haliwezi ishinda hii vita, kwa kua wana dhahabu wawakidi Wagner PMC.
 
Amani haipatikani ila Kwa UPANGA TU. ( Peace through strength).

Ondoa Majeshi ya KIMATAIFA huko... Ruhusu Mchina na Mrusi wakusaidie.

Ingiza Majeshi ya Nchi Rafiki , Jiimarishe Kisilaha, Kifedha .

Fanya Counteroffensive ya Nguvu , Piga piga mpaka uingie Rwanda, endelea kupiga tu Kwa Kila atakayeingia 18 awe ni Uganda muunganishe kwenye kichapo.

Siku Congo atafanikiwa kumpa Maumivu Mnyarwanda, mbona atakua mezani tu.

Shida Moja itakayobaki ni RC .
Mkuu, unafikiri ni rahisi kushawishi viongozi wa nchi rafiki wakupe msaada wa Kijeshi? Unafikiri viongozi wa Congo DRC hawakuwahi kujaribu kutafuta support ya kijeshi kutoka nchi marafiki?
 
Congo kuwa na amani ni Mungu kuchukua utajiri wote aliouweka kwenye ardhi ya Congo. Watu wanailaumu Rwanda na Uganda bila kukumbuka Lumumba aliuwawa na mabeberu kwa baraka zote za UN... Wanufaika halisi wa utajiri wa DRC ni mabeberu.. Rwanda na UG ni puppets tu. Zambia na TZ ni matajiri pia ila kinachotusaidia ni kwenda sawa na mabeberu.
 
Ni kuomba msaada wa Wagner alafu mnatembeza kiboko mpaka Rwanda ,Uganda akiingilia mnaunganisha kwenye kipigo mpaka Entebe ni hapo mtashangaa hata wale mbilikimo wa misitu ya Congo watajitokeza kuwa ni binadamu sio kitoweo
Unaweza ukafafanua kidogo kuhusu Mbilikimo wa Congo?
 
Ningefanya mabadiliko ya majenerali wa jeshi na kusimika kambi za makomando hatari huko kwenye ngome ya M23.
Nikishasafisha M23, nasimika kambi za makomandoo wa kijeshi kwenye mipaka ya Rwanda, Burundi na Uganda yaani huko mipakani hakuna paka yoyote kukatiza kuingia DRC
 
Kama ungelikuwa Rais wa Congo DRC, ungeweza kuifanya hiyo nchi kuwa na amani?

Naamini suluhisho la Congo DRC lipo kwa Wacongoman wenyewe! Lakini hilo wataweza kulifikia kupitia viongozi wao, kama wasemavyo "wahenga", "Everything rises and falls under the leadership"

Ingelikuwa wewe ndiye Rais, ungelifanyeje ili nchi yako ya Congo DRC iwe na amani ya kudumu?
Kwanza kuwapa elimu ya daraja la juu Wa Congo man kuwapa ujasr na kuipenda nch yao kwa nguvu zao zote chapili kuweka sheria na sera ya maamuz magumu, cha tatu kujenga jesh imara na enye nguvu na high technology, cha nne kuunganisha wacongo man wote, cha tano kulinda na kusimamia rasimali zote za nch kikamilifu na kuelekeza nguvu kubwa sehem enye migogoro ya mda mrefu, kwa mfano kivu mashariki kuweka vikos kila kilomita 15 kuwe na kambi ya jesh, kubwa lenye ulinz wa hali ya juu kuwa na usalama wataifa kila sehem za nch. Kungowa na kuchoma mizz yote ya viongoz walio pita na kuunda Congo superpower isyo lega laga na kila mwananch hanahaki kikatba kuilinda nch yake kwa mabaya yote yatakayo leta was was wakuvunja aman na kukataza starehe na kujikita kweny kuijenga nch kwa kilimo ufugaji kuwa sehm ya kila mtu kuwajibika ipasavyo
 
Nahisi hata Rais aliyepo sasa tayari kaitwa katulizwa, kaambiwa na mabeberu '... kaa kwa kutulia chuma kiasi unachotaka, subiri muda wako uishe alafu tembea'.

'Ukileta zako humalizi muhura hapa'

Ndiyo maana mzee Tshieked kapoa sana, vinginevyo ule moto alioanza nao ulikuwa wa maana sana, nilidhani ungemfikisha mahali angeweza kufanya maamuzi hata ya kuwaleta Wagner.

Afrika bado ni colonies japo kwa nje tunaonekana tunajitawala.

Nchi yoyote inayoonyesha kupevuka inaminywa irudi chini na hao wakoloni weupe.
 
Kwanza nafunga mipaka na maadui na kuweka demillitirazed zones na land mines za kutosha. Baada ya hapo naanza kusaka wa ndani mmoja mmoja. ADF, M23 na wakorofi korofi wote.
 
Hakika, yule dogo wa Burkinabe wanataka kumuua wafaransa.
 
Kwanza nafunga mipaka na maadui na kuweka demillitirazed zones na land mines za kutosha. Baada ya hapo naanza kusaka wa ndani mmoja mmoja. ADF, M23 na wakorofi korofi wote.
Unapiga mkaa wote sijui ADF, M23 na wapuuzi wote kutoka Uganda na Rwanda halafu unafukuza majeshi yote ya kinafki ya kulinda amani hakuna cha maana wanachofanya.
 
Unapiga mkaa wote sijui ADF, M23 na wapuuzi wote kutoka Uganda na Rwanda halafu unafukuza majeshi yote ya kinafki ya kulinda amani hakuna cha maana wanachofanya.
Siku akipatikana kiongozi atakayewaunganisha Wakongoman na kuwa kitu kimoja, hakutakuweko na atakayeweza kupenyeza pua yake pale!

Mbona Wavietnam waliweza? (Usiniulize kivipi kwa sababu ninayoyajua kuhusu Vietnam ni machache sana. Nimesikia wana umoja mno na ni wazalendo sana kwa nchi yao).
 
Back
Top Bottom