Ungekuwa kwenye nafasi hii, ungefanya maamuzi yapi?

i appreciate ths👍
 
Msiwe mnatuletea visa ambavyo mwisho wa siku utata unajulikana upo wapi. Hapo wote wameleta mambo ya kisenge....

Mwanaume ndie kaanza kuleta ufala, unasafiri kwenda taifa la mbali sawa ila sasa unaanzaje kuleta ukimya usio na sababu, inamaana hakukuwa na means za kuwasiliana hata kwa Facebook...... Huo si ufala...

Na huyo demu yeye ameshatambulishwa ukweni, miaka miwili yote hakwenda tena ukweni kuwajulia hali ikiwamo kuulizia habari za jamaa....?!

Conclusion:

Acheni kuleta visa au story za kutunga ambazo hazizingatii uhalisia huo ni ufala maana mtu akisoma badala ya kuelimika au kujifunza anapata maudhi...... Coronavirus itusumbue vichwa bado na huu upuuzi pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Relax..!
Usikariri maisha..!!
 
Unataka sema stori haijakamilika?


 
Mistari ya mwisho nadhani ina majibu ya maswali yako, hivyo ndivyo nilivyoamini pia ila huwezi mshauri hivii mtu aliyependa akakuelewa, Cc; Chindy..!

Turudi kwenye mada.!
Mm ningemwambia kila kitu before anything.

Hivi hii ni nini ati? Zamani nikiwa mjinga full uaminifu hata no sitowi, basi ningemchamba huyo binti aliezaa mpaka basi.
Ila baada ya kunyooshwa na the so called uaminifu hasa kwa hao viumbe waishio mbali sana ahaaaa nani afanye maujinga hayo?

Wewe mwambie ajiamini amwambie ukweli kizuri wote wana watoto, akimuacha its ok.uwezi juwa mtu kumkatia mawasiliano alikuwa na nani huko? Hiyo inaitwa kubalance shobo. You never know with men.

Tujifukize jamani.
 
Mimi kama Mimi ningekuwa binti ningekutana na jamaa alafu nampiga chini apoapo kama angeleta habari za mapenzi ingeniuma Ila ingemsaidia mbeleni kuliko ajiweke kwake tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kumwambia ukweli jamaa aamue kusuka au kunyoa. Na wala asienze kumshutumu kwa kosa la kutokuwa na mawasiliano maana hata wangekuwa wanawasliana bado angetokea mtu wa kumtuliza vinavyowasha na huenda bado mimba ingetokea. Miaka miwili ni mingi hata kwa wanandoa ni ngumu kuvumilia lazima mambo yataharibika tu. Jaribu kufuatilia watu wenye mahusiano ya aina hii unaowafahamu wangapi walivumilia bila kucheat. HAKUNA.

Long distance relationship ni shetani na ni sawa na kukimbiza upepo lazima utaumia tu. Unaweza kuta jamaa naye ameacha watoto kule sema kwake tayari mtoto ataonekana kwa kuwa wako nchi moja. Kama anaipenda damu yake amuambie ukweli tu. Mtoto wake ana thamani kubwa kuliko ndoa inayokuja yenye wasiwasi mwingi wa kugundulika. Miaka miwili mko mbali bila mawasiliano mtu akicheat hakuna kulaumiana hiyo ipo tangu jadi.

Wazee walienda kufanya kazi Johannesburg kwenye migodi enzi hizo na sehemu zingine za Zimbabwe au msumbiji, na kutokana na aina ya miundombinu ya usafiri kuwa duni wakati huo walikaa zaidi ya miaka miwili wakiwa ughaibuni. Na waliporudi walikuta wake zao wana watoto. Walikalishwa chini na maisha yaliendelea ingawa kwa sasa kuna ugumu. Lakini ampe thamani mtoto kuliko ndoa maisha mengine yaendelee. Kama ipoipo tu.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mistari ya mwisho nadhani ina majibu ya maswali yako, hivyo ndivyo nilivyoamini pia ila huwezi mshauri hivii mtu aliyependa akakuelewa, Cc; Chindy..!

Turudi kwenye mada.!
So nikirudi nita kukuta na....?
 
Ilo mbona lipo wazi kwa wanaume 99% kama sio wote.


Mimi Ningemwacha tu hamna namna ...namuacha sababu ameufanya ujinga akiwa tayari yuko pamoja namm.




Huwa nasema ivi...Heri kuoa mwanamke ulomjua akiwa tayari ni mwenye mtoto/watoto.... Kuliko kuoa mwanamke ulomjua akiwa hana mtoto, Ila baadae akabeba ujauzito wa mwingine tena mkiwa bado pamoja.



Hapo bidada, nikusema ukweli tu kisha apambane na hali yake.


Kwa sababu Nina imani, hatokaa kumficha Mtoto, nasiku jamaa akiujua, basi watagombana sana hata kuachana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…