Ungekuwa na mtaji ungeagiza nini kutoka nje ya nchi?

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2015
Posts
1,527
Reaction score
3,811
Wakuu tubadilishane mawazo hapa

Tusio na mitaji huwa tunakuwa na mawazo mazuri sana ya kibiashara.

Kwa mfano, mimi napenda sana kuagiza shela za harusi kutoka China na Dubai kwakuwa bei zao zipo chini sana.

Gauni zuri la harusi China linauzwa kwa pesa ya kitanzania laki na nusu mpaka laki mbili na mpaka linafika Dar halizidi laki tatu. Lakini wafanya biashara wanauza kuanzia laki tano mpaka milioni moja.

Kukodisha wanaanzia laki na nusu mpaka laki tatu hivyo faida yake ni kubwa, sema tatizo mitaji.

Je, wewe ungekuwa na mtaji ungeagiza bidhaa gani kutoka nje ya nchi.?
 
Kma unafrem kkoo agiza vitu vidogo vidogo vya simu kma charge vioo betri nk utatengenez ela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…