Ungekuwa Rais wa Congo ungefanya nini kumaliza migogoro ya kivita?

Ungekuwa Rais wa Congo ungefanya nini kumaliza migogoro ya kivita?

musicarlito

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2020
Posts
591
Reaction score
909
Wasalaam wakuu,

Congo inabembekeza ubia wa kumiliki madini na Marekani ili ipewe Usalama kama malipo

Binafsi nadhani Congo ukitoa Lumumba Patrice haijawahi kuwa na kiongozi wa kweli mzalendo anaeipenda nchi yake. Hali hii imeambukiza taifa zima na hasa vijana ambao ni nguvu kazi. Wote wanaota kwenda Paris, waache nchi yao yenye utajiri wa rasilimali waende kwenye nchi za watu

Nchi ipo kwenye shida vita asilimia kubwa ya vijana wapo kwenye muziki na magitaa wengine kwenye michezo nk

Congo is a failed state, mkataba wowote unaohusu madini na nchi za magharibi, lazima Congo itajutia.
 
1. Ningewatambua raia wote wa nchi bila kubagua watusi
2. Ningewapa uraia wahutu waliopo drc na kuwasihi waachane na visasi vya mauaji
3. Maendeleo napeleka kote sio kinshasa tu
4. Ujirani mwema, sifugi waasi wa kumpindua jirani
5. Madini nawapatia mabeberu wachimbe wanipe kodi kidogo
6. Miundombinu ya nchi nzima inakuwa kipaumbele cha kwanza
7. Nawekeza kwenye jeshi na wanajeshi
8. Nasisiza kazi kuliko starehe na kijichubua
9. Najenga congo iliyo serios na watu serious
10. Ukila rushwa unapigwa shaba hadhani kwenye tv ya taifa
 
Namba 1 na 2 sidhani kama ni rahisi sana
 
Kuwatambua raia wote walioko mashariki mwa Congo hasa miji ya Kivu kusini na kaskazini, Uvira, wakazi wa milima ya Mulenge(Banyamulenge), Goma, Kisangani, Virunga kama raia halali wa DRC bila kujali mila, desturi na tamaduni zao. Pia kuwashirikisha wakazi hao kwenye maendeleo na ujenzi wa Congo mpya.
 
Nipe elimu kidogo mkuu, hao watusi wanabaguliwa vipi?
 
Kuwatambua raia wote walioko mashariki mwa Congo hasa miji ya Kivu kusini na kaskazini, Uvira, wakazi wa milima ya Mulenge(Banyamulenge), Goma, Kisangani, Virunga kama raia halali wa DRC bila kujali mila, desturi na tamaduni zao. Pia kuwashirikisha wakazi hao kwenye maendeleo na ujenzi wa Congo mpya.
Nimetoka kumuuliza mwenzio, hao Wanyamulenge kivipi hawatambuliwi? Yaani wanafanywaje? Nieleweshe na wewe.
 
Mgogoro kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kundi la M23 ni miongoni mwa migogoro sugu katika eneo la Mashariki ya DRC, na umetokana na mchanganyiko wa sababu za kisiasa, kijamii, na kijiografia. Ili kutatua mgogoro huu, kuna hatua kadhaa ambazo DRC na jamii ya kimataifa zinaweza kuchukua:
  1. Mazungumzo na Diplomasia😀RC inaweza kuendelea na jitihada za kufikia suluhu kwa njia ya mazungumzo na M23, ikiwa ni pamoja na ushirikiano na nchi za majirani kama Rwanda na Uganda ambazo zinahusishwa na mgogoro huu. Hili linaweza kufanikishwa kupitia majadiliano ya kisiasa na kupitia mashinikizo kutoka kwa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, na Mashirika ya Kikanda kama EAC (East African Community).
  2. Kujenga Uaminifu:Kuepuka vita zaidi na kuhakikisha kwamba pande zote zinaheshimu mkataba au makubaliano ya amani yanahitaji kujenga uaminifu. Hii ni pamoja na kuhakikisha kwamba wawakilishi wa M23 wanahusishwa kwenye mchakato wa kisiasa kwa namna ambayo inahakikisha usalama na haki za makundi yote, ikiwa ni pamoja na wakimbizi na raia wa DRC.
  3. Kuimarisha Usalama wa Raia:Serikali ya DRC inaweza kuongeza juhudi za kuhakikisha usalama wa raia wake, hasa katika maeneo yaliyoathirika na makundi ya waasi. Hii itahusisha kuimarisha shughuli za vikosi vya usalama na kuhakikisha kuwa wanajeshi wa Umoja wa Mataifa na vikosi vya kikanda kama vile FIB (Force Intervention Brigade) wanahusika zaidi katika kulinda raia na kupambana na vikundi vya waasi.
  4. Ufadhili wa Kimataifa na Msaada wa Kiuchumi:Nchi za kimataifa na mashirika ya misaada yanaweza kutoa msaada kwa DRC katika kuimarisha uchumi na usalama. Kwa mfano, kusaidia katika kurudisha ustawi katika maeneo yaliyokumbwa na vita, ikiwa ni pamoja na elimu, huduma za afya, na ajira, ili kuzuia makundi ya waasi kama M23 kuajiri vijana kutoka kwenye familia maskini.
  5. Matumizi ya Vikwazo na Shinikizo la Kimataifa:Nchi za kimataifa, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa, Marekani, na Umoja wa Ulaya, zinaweza kutumia vikwazo dhidi ya viongozi wa M23 na wafadhili wao ili kuwalazimisha kukubaliana na mchakato wa amani. Hii inaweza kusaidia kupunguza rasilimali zinazowawezesha waasi kuendeleza shughuli zao.
  6. Kurejesha Mchakato wa Amani wa Kinshasa:Serikali ya DRC inaweza kuendeleza na kuimarisha mchakato wa amani wa Kinshasa (au mikataba mingine inayohusisha pande zote) kama njia ya kuhusisha pande zote zinazohusika. Hii ni muhimu katika kutoa nafasi kwa waasi kujumuika kwenye mchakato wa kisiasa na kuondoa misuguano ya kijeshi.
Mgogoro wa M23 ni changamoto kubwa, lakini kwa ushirikiano wa kimataifa na hatua za ndani, DRC inaweza kupata suluhu ya kudumu. Hata hivyo, ni muhimu kuona kuwa hali ni ngumu na inahitaji mbinu za muda mrefu za kuhakikisha amani na ustawi kwa wote.
 
Wanaambiwa warudi kwao Rwanda
Yaani mtusi yeyote DRC anaambiwa arudi Rwanda?

Je hao watusi ni raia wa Congo au wakimbizi?

Utamwambiaje mtu mwenye vielelezo halali vya uraia aende nchi nyingine?

Wananyimwa kazi? Hawapewi huduma za kijamii? Kwani wanakaa sehemu moja?

Hii changamoto ni kwa utawala huu tu ama ni maraisi wote waliopita?
 
Mpaka wa wazungu uliwakata wakajikuta drc, ila kwasababu wana mila za Rwanda na wanaongea kinyarwanda ndo wanaambiwa warudi Rwanda. Wanasema hakuna mkongo anaeongea kinyarwanda
 
Kisheria mtoto akizaliwa mahali popote duniani ni raia wa hiyo sehemu alipozaliwa. M23 wengi wao wamezaliwa Congo basi ni raia wa Congo. Nijibu swali! Nitazungumza na m23, tuelewane na maisha yaende.
 
Back
Top Bottom