Ungemshauri nini Col.Gadafi

Ungemshauri nini Col.Gadafi

WembeMkali

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2007
Posts
282
Reaction score
3
Kama ungepewa fursa ya kutoa mawazo yako kwa Mwenyekiti mpya wa AU mheshimiwa Col.Gaddaffi ungemshauri nini?

-Ni upi msimamo wako kuhusu suala la nchi za kiafrika kulipwa fidia na mataifa yaliyowatawala? kama Japani ililipwa/inalipwa fidia na marekani kwa mashambulizi ya mabomu ya kiatomic kuna ubaya gani kwa nchi za kiafrika kutolipwa chochote?

-Ni upi msimamo wako wa kuzikaribisha nchi za Carribean kwenye umoja wetu wa kiafrika.Hasa ukizingatia nchi hizo nyingi zina asilimia kubwa ya watu kutoka Afrika?

-Hivi ni kweli kuwa suala la United states of Afrika ndilo suluhu la matatizo ya Afrika? nini kifanyike kama viongozi wetu hawataweza kuafikiana kuhusu hilo?

-Kuna mataifa mengi ya ulaya ambayo yanainterests kubwa katika bara la Afrika
e.g Ufaransa,Marekani,Ubeligiji,Ureno,Uingereza n.k na kwa miaka mingi yamekuwa ndiyo chanzo kikubwa cha migogoro ndani ya bara hili.Je ungependa mwenyekiti mpya wa AU achukue hatua gani kuhusu hili hasa ukizingatia kuwa hakuna kiongozi hata mmoja wa kiafrika( labda Mugabe) anaweza kukemea mataifa haya kwa vitendo vyao vya kizandiki.

Wembe.
 
Umoja wa Afrika ndiyo suluhu pekee kwamatatizo ya Afrika.
Viongozi wetu wamekwishaafikiana kuwa wanataka Muungano. Wanabishana kuhusu jinsi,na lini.
 
Umoja wa Afrika ndiyo suluhu pekee kwamatatizo ya Afrika.
Viongozi wetu wamekwishaafikiana kuwa wanataka Muungano. Wanabishana kuhusu jinsi,na lini.

Je ni kweli wako tayari ku-give up their powers?...
 
Umoja wa Afrika ndio suluhu ya matatizo yetu,pia kuzikaribisha nchi za karibiani ni wazo zuri zaidi ili tuwe na himaya kubwa zaidi.Ukweli ni kwamba Afrika ilikuwa moja kabla ya wakoloni kuigawanya ili waweze kuitawala,pia ni lazima wakoloni watulipe fidia,kwa yote waliyotufanyia manake ulikuwa ni uzandiki na unyonyaji wa hali ya juu.Pia ni lazima kuzikemea nchi zinazoingilia mambo ya ndani,ya nchi zetu.Ushauri wangu ni kwamba lazima tuungane ili kuweza kuwa na sauti moja,,,,,,
 
Ningemuuliza,
"ivi uzalendo wako ni kwa muungano wako na waArabu, ama kwetu - barani mwako - Afrika?"

"ivi, nia zako za kuunganisha waAfrika, ni za kusaidia bara la Afrika ama kusaidia marafiki zako tokea zamani, muungano wa waArabu?

"Utauza mafuta bei chini kwa ndugu wa bara lako, wakati OPEC ikinyanyusha bei baada ya kupandishwa hasira na waUlaya ?"
 
Back
Top Bottom