Ungependa kuzaa mtoto wa maabara? Basi wanasayansi wapo Maabara

Ungependa kuzaa mtoto wa maabara? Basi wanasayansi wapo Maabara

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Wanasayansi wanaendelea kutafiti kisayansi kuhusu njia mpya ya uzazi itakaotumika kutengeneza mtoto maabara bila kufuata njia za kawaida za uzazi zinazohusisha ubebaji wa mimba na kuzaa.

Njia hii inaenda mbali zaidi, kuliko inayotumika sasa, ambayo mwanamke anaweza kupandikizwa mbegu na kuzaa, bila kujamiiana.

Wanasayansi hao wanachokifanya sasa ni kutengeneza mfuko wa uzazi wa binadamu nje ya tumbo lake katika kizazi kijacho ama viwili, wakiamini, matokeo ya utafiti huo yataibua hisia mseto kuhusu hatua hiyo inamaanisha nini kwao wanasayansi lakini pia kwenye maisha ya mwanadamu.

Njia hiyo mpya inayotafutwa inalenga kujali hali na afya za wanawake wanaobeba ujauzito, wanaotumia muda mwingi kulea ujauzito na kuathiri miili yao mpaka wakati wa kujifungua.

Utafiti huu unaitwa kisayansi 'artificial womb', unaofanywa na wanasayansi mbalimbali duniani wakiwemo kutoka Chuo kikuu cha Oslo, Norway, Chuo Kikuu cha teknolojia Eindhoven cha Uholanzi , Chuo Kikuu cha Singapore, na Taasisi ya sayansi ya Weizmann nchini Israel.

Je, hatua hii ya kutengeneza mfuko wa uzazi maabara imefikia wapi?
Wanasayansi duniani kwa sasa wanahaha kutengeneza mfumo unaofanana na uterasi ya mwanadamu, lengo ni kufanya mfumo huweze kubeba na kutunza mtoto sawa na mfumo wa mwanadamu. Kwa mujibu wa wanasayansi hao, hilo linawezekana kufanyika kwenye mashine za kawaida za joto (incubators).

Majaribio ya utafiti huo yamefanyika kwa kutumia kondoo na kufanikiwa.

Kile tunachokifanya ni kuunganisha mirija miembamba sana kwenye kitovu na kufanikiwa kupitisha damu kipitia mirija hiyo, na hilo linatusaidia kupeleka hewa kwenye fetasi, bila kuthitajika kutumia mapafu kufanya hivyo', anasema Dr Mathew Kemp, mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Singapore.

Utafiti huo umejielekeza kusisimua mifumo ya uzaizi kwa kutumia kompyuta itakayoendesha roboti maalumu yenye mfanano wa mfumo wa mwanadamu.

Jamii imepokeaje utafiti huu unaofanywa?
Wako wanaoona utafiti huo, unakwenda mbali zaidi. Wengi wanaona, kunahitajika kuzingatiwa kwa maadili ya kisayansi katika kupatikana kwa matokeo yake.

Lakini watafiti wenyewe hawana shaka na wanachokifanya.

'kwa mara ya kwanza mwaka 1979, mtoto wa kwanza alipopatikana kwa njia ya upandikizaji ya IVF, kuliibuka hoja nyingi, kwa hiyo ni kawaida ukisikia watu wanasema tunaenda mbali ni hatari, anasema Dr. Anna Smajdor kutoka Chuo Kikuu cha Oslo.

Mwandishi mwandamizi wa masuala ya kisayansi, Helen Sedgwick Helen anasema jambo zuri kwanza kabla ya kuangalia athari katika mifumo ya maisha ya mwanadamu aliyoizoea, ni kwamba wazo hilo limepokelewa vyema na jamii.

'kwangu mimi, hili naliona kama suluhu kwa binadamu, itaokoa maisha ya watoto wengi ambao hufariki kabla ya kuzaliwa, inaweza kubadili maisha ya watu ambao hawana uwezo wa kubeba mimba na kuzaa kwa njia ya kawaida',

Hoja yake inaungwa mkono na Dr. Anna Smajdor ambaye anaongeza kuwa, 'tunaishi kwenye maisha ambayo, mwanamke, yuko kwenye msukumo mkubwa wa kutekeleza masuala ya mila na utamaduni, lakini kinacholeta mabadiliko sio maendeleo haya ya kisayansi, ni muitikio wa jamii yenyewe.

Pamoja na hatua hii maswali makubwa anayojiuliza Mwandishi Helen ni kwamba, nani atakuwa mmiliki wa teknolojia hii ya kuumba binadamu nje ya mifumo ya kawaida ya uzazi? Nani atakayeidhibiti? Na je itakuwa maalumu kwa watu gani?au watu watalazimishwa kuitumia?

Je teknolojia hii ya kuumba binadamu maabara ikifanikiwa, italeta mabadiliko gani?
Kwa mara ya kwanza watafiti waliweza kufanikiwa kuumba kisayansi kiini tete cha panya katika tumbo la nje liliotengenezewa maabara kwa muda wa siku 11 pekee. Walikuwa wanajaribu kuangali namna gani ogani za panya zinavyozalishwa na kukua, hatua ambayo inawezekana tu kama kiini tete hicho kinakuwa ndani ya tumbo.

' tumeanza kufanyia kazi utafiti huu kupitia wanyama wengine ambao wanafanana mifumo yao ya uzazi na viini tete na binadamu , mmoja wapo ni sungura, na naweza kusema kwa kweli matokeo ya utafiti yamekuwa ya mafanikio sana, kukiwa na vitu vichache vya kufanyia kazi', anasema Dr. Jacob Hanna kutoka Taasisi ya sayansi ya Weizmann na kuongeza, ' matokeo haya, yanatupa moyo kwamba, inawezekana pia kwa binadamu kufanyika hivyo'.

Wanasayansi wanaona hii ni suluhu, na italeta mabadiliko makubwa ya kuokoa watoto wanaozaliwa wiki 23 na chini ya wiki 25.

Unajua unapoleta kitu kipya kama hiki, kinapaswa kuwa na ubora kuliko vilivyokuwepo, ukiangalia wastani wa kuishi kwa kiumbe chenye wiki 23 ni aslimia 40% au 50%', anasema Dr Kemp.

Ingawa kuna hoja mchanganyiko kuhusu hatua hii ya kuumbwa kwa binadamu maabara, watafiti wenyewe wanasema, upo uthibitisho kwamba, faida ya kufanya hivi ni kubwa zaidi kuliko hasara.

Watafiti hao wanakadiria kwamba katika kipindi cha miaka 10 ijayo, wataanza rasmi majaribio kwa binadamu, huku wakiendelea kuruhusu mijadala ya kuboresha adhma yao hiyo.
 
wanatuletea artificial human being, itakuwa balaa huko baadaye.... kuzaa bila kupigana miti?
 
😂😂😂 nilikua nawaza kwa sauti mkuu
Kwa kweli inafikirisha sana mkuu,Sasa tutaambia Nini watu wa Dini maana wao vitu kama Hivyo wanaona mauza uza tu na venye wameaminishwa Mungu humuumba mtoto tumboni Kwa mama baada ya mbegu kukutana Sasa safari hii sijui watasema Nini maskini!
😁😁😁😁🔥
 
Kwa kweli inafikirisha sana mkuu,Sasa tutaambia Nini watu wa Dini maana wao vitu kama Hivyo wanaona mauza uza tu na venye wameaminishwa Mungu humuumba mtoto tumboni Kwa mama baada ya mbegu kukutana Sasa safari hii sijui watasema Nini maskini!
😁😁😁😁🔥
watasema ni matukio ya siku za mwisho😄
 
Back
Top Bottom