Kwa mtazamo wangu,
a. Migomo isiyo ya lazima isitokee
-- Sisi kama wazazi tunaangusha watoto wetu hatuwafundishi mentality ya kujitegemea wakati wanakua. Mtoto likizo kazi kuzurura au kukaa tu nyumbani na kusubiri kulipiwa kila kitu. Inabidi mentality ya kijamaa itoke kwenye jamii yetu watu wawe watafutaji (wazazi kwa watoto) ili mtoto hadi anafika chuo kikuu anajua thamani ya elimu anayotafuta na ugumu wa maisha yalivyo hivyo kama haki yake atadai kwa nguvu lakini atajua na waibu wake. Utakuta sehemu kama cafeteria pale wanawahudumu ambao sio wanafunzi sasa nini kinazuia mwanafunz mmoja kuomba kazi hata shift ambayo hana vipindi. Vijana wetu wakifika chuo kikuu status quo inawaharibu utakuta mda wanao wakutosha lkn ukifika mtihani hawajajiandaa kwahiyo wanadesa lkn mi naona yote hii ni kwasababu tu hawakujifunza jinsi ya kutafuta kitu katika life.
-- Wanafunzi wa vyuo vikuu wajue wameenda pale kutafuta maisha sio "Sunday School", so time is of the essence especially to them maana ulimwengu na opertunities havisubiri mtu. Ukiangalia vijana wetu wengi siku hizi wanaona chuoni ni kama sehemu ya kukulia kwahiyo wakipata tatizo tu huwa wana option mbili moja kuongea na uongozi wakikataliwa wanachotaka wanagoma.
b. Elimu ya Juu inapatikana kwa kila atakaye
-- Kila anayetaka awe tayari kuitafuta, kama mtu anajua kuwa mwaka flani mwanangu atakuwa anaingia chuo kikuu na zitahitajika kiasi fulani kwa ajili ya 40% ya mkopo atatafuta. Kwa wale wasio na uwezo wengine watakosa wengine waende kwenye vyuo ambavyo vitawawezesha kujitegemea mapema zaidi. Tatizo la wengi wetu watanzania kujituma na kujitegemea kudogo kila mtu anataka akaajiliwe akitoka chuo kikuu. Familia zifanye strategic planning badala ya kumsomesha mtu diploma ya banking waangalie uwezekano wa yeye kusomea FTC au kitu kama hicho ambacho akitoka hapo anaweza hata kutengeneza vigoda au akajiingiza kwenye shughuli za ujenzi ambazo asilimia kubwa zinafanywa na watu wasio na ujuzi huo kwahiyo atakuwa na advantage huko.
-- Tujidai kuwa wakati tunapata uhuru nchi nzima ilikuwa haina uwezo wa kujisomesha, then serikali ikaja ikasomesha watu, sasa hawa waliosomeshwa tulitarajia wao ndio wawe washauri wazuri wa ndugu zao (watoto, wajomba,shangazi) waliobaki kule kijijini au katika hali ya umaskini. Lakini hamna kitu kama hicho hadi leo wanafunzi wetu wanafikiria kama walivyokuwa wanafikiria wanafunzi wa mwaka 1990, ukiangalia kisa ni umimi. Wale waliosoma hawakuweza kuwashauri wenzao (ambao ni ndugu zao) kwamba nyakit zinabadilika na approach kwenye elimu ibadilike. Ukiangalia vitu walivyogomea watu mwaka 1992 ndio hivyo hivyo wanavyogomea mwaka huu hii inaonyesha watu waliomaliza toka mwaka huo 1992 walipoingia serikalini au makazini walijitoa kuwa wadau waelimu ya juu. Yaani kwasababu wao washapita sio tatizo lao tena maana kama wasingekuwa wa mimi aidha sera zingebadilika au mtazamo wa jamii ungebadilika.
c. Familia zinaweza kumudu elimu ya juu
----Huku Ulaya utakuta mtoto anazaliwa na mzazi anafikiria mwanangu ataendaje chuo kwahiyo wanaanza savings kwa ajili ya kitu kama hicho, huku kwetu wat wengi watasingizia umaskini lakini ukweli ni kwamba ndio maskini wapo lakini kuna sehemu kubwa tu jamii wanaofanya mambo ambayo sio lazima (mfano baba kila siku lazima apitie kilabuni na kupata fegi moja mbili) ambapo kama angekuwa na mipango na marengo bora ya kusomesha mwanae engepunguza vitu visivyo lazima. Ni jukumu letu kama wazazi kuanza kujipoanga mapema, wale wanaoshindwa kabisa watakuwepo na hawakosi katika kila jamii. Kwahiyo wenye uwezo wakiweza kutafuta vyao ndio tutapata nafasi ya kuwa identify na kuwasaidia wasio nauwezo. Tatizo lililopo sasa hivi wakati wa mgomo wote wanajiita watoto wa wakulima lkn ukiangalia maisha wanyoishi wakiwa na fedha utakuta 10% au zaidi ndo wanaishi kama watoto wa wakulima walio vyuo vikuu.
Kwasasa ni hayo tu mzee