Mi ningekuwa mbali zaidi ya hapa .Sasa hivi ndio najifundisha na bahati nzuri na mtoto.Najitahidi kumuelewesha kitu fulani kwa kuzungumza nae na unagundua ni shida ndogo tu ,mnatatua maisha yanaendelea.Mtoto kagoma kula chakula fulani watu washanyanyua magongo wanachapa kumbe unaweza kuzungumza nae ukajua labda alienda sehemu akawa na experience mbaya na huo msosi.
Tumekuwa kwa maisha ya hofu hofu tu mtu hata hujiamini,huwezi kufanya mawasiliano sawa sawa kwa hayo hayo maviboko.
Mwanangu nataka awe na fikra huru,aweze kuwasiliana sawasawa,ajiamini.Skills ambazo baba yake nilizikosa na siamini kama mijeledi itanisadia.