Ungeweza kusafiri kwenye muda, ungeenda miaka ya mbele au ya nyuma? Jambo gani ungelifanya?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Mi binafsi ningechukua Tsh. 1m, ningeweka fixed halafu ningeenda mbele kama miaka 100 kula faida.

Wewe ungefanya nini, kitu gani ungebadilisha?
 
Aiseee....ningerudi nyuma hadi miaka ya 2000, ili nikapige story na ndugu, jamaa na marafiki zangu ambao now hawapo tena duniani.
Ningewapelekea zawadi na story za 2020 na 2021.
 
Ningerudi nyuma 2004..... Niongee na maza, tupige story mingi sana.. Nimuulize maswali mengi mno
.... Kila kukicha namkumbuka yule MAMA sijawahi kupenda kiumbe kingine zaidi yake na kama nitazaliwa tena naomba nizaliwe na yeye pekee R. I. P Mom
 
Ningalirudi nyuma mpk kwa adamu na Eva wake nikawatie adabu kwanini walikula Yani sijui wakoje tu ile couple..😎
 
Ningeenda mbele mpaka mwaka 2030 niione Nchi yangu ita kuwaje
 
Mi binafsi ningechukua Tsh. 1m, ningeweka fixed halafu ningeenda mbele kama miaka 100 kula faida.

Wewe ungefanya nini, kitu gani ungebadilisha?
Kwa upande wangu mimi, ningekuwa na u-rewind muda katika kipindi kile tu ambacho baba yangu mzazi alikuwa hai!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…