UNICEF: Kila dakika '1:40' mtoto au kijana chini ya miaka 20 anaambukizwa UKIMWI

UNICEF: Kila dakika '1:40' mtoto au kijana chini ya miaka 20 anaambukizwa UKIMWI

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Takribani kila dakika moja na sekunde 40, mtoto au kijana chini ya umri wa miaka 20 alikuwa anaambukizwa Virusi Vya UKIMWI, VVU mwaka jana 2019, na kufanya idadi ya watoto wanaoishi na VVU kufikia milioni 2.8, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema katika ripoti yake iliyotolewa mjini New York Marekani na Johannesburg Afrika Kusini.

Ripoti hiyo, kwa jina Ufikiriaji mpya ushughulikiaji VVU wenye mnepo kwa ajili ya watoto, barubaru na wajawazito wanaoishi na VVU, inaonya kuwa watoto wanaachwa nyuma katika vita dhidi ya VVU. Jitihada za kuzuia na matibabu kwa watoto yanabaki kuwa ya chini kabisa miongoni mwa watu muhimu walioathirika.

Katika mwaka 2019, si zaidi ya nusu ya watoto watoto ulimwenguni kote walipata matibabu ya kuokoa maisha, ambayo yanazorota kwa akina mama asilimia 85, na watu wote wazima wanaoishi na VVU asilimia 62. Takribani watoto 110, 000 walifariki kwa UKIMWI katika mwaka huo wa 2019, imeeleza taarifa ya UNICEF.

Katika miezi ya Aprili na Mei, sanjari na kufungwa kwa mipaka, matibabu ya VVU kwa watoto na upimaji wa virusi kwa watoto katika nchi zingine ulipungua kati ya asilimia 50 hadi 70, na uanzishwaji mpya wa matibabu ulipungua kwa asilimia 25 hadi 50.

Takwimu za ziada 2019 zilizojumuishwa katika ripoti

Watoto 150,000 wenye umri wa miaka 0-9 walikuwa wameambukizwa VVU hivi karibuni, na kufanya idadi ya watoto katika umri huu wanaoishi na VVU kufikia milioni 1.1. Vijana 170,000 wenye umri wa miaka 10-19 waliambukizwa VVU hivi karibuni, na kufanya idadi ya vijana wanaoishi na VVU kufikia milioni 1.7.

Wasichana 130,000 waliambukizwa VVU mnamo 2019, ikilinganishwa na wavulana 44,000. Jumla ya vifo vinavyohusiana na UKIMWI vya watoto na vijana vilikuwa 110,000; 79,000 wenye umri wa miaka 0-9 na 34,000 wenye umri wa miaka 10-19.


 
Toka wasemage tungekufa kama kuku na maiti kutapakaa mitaan sabab ya covid19

Huwa siwaamin hao nyau...kwanza wengne hzo takwim wanatumia kupigia hela.huko huko UN...wanasingizia ili wapewe pesa ..
 
Toka wasemage tungekufa kama kuku na maiti kutapakaa mitaan sabab ya covid19

Huwa siwaamin hao nyau...kwanza wengne hzo takwim wanatumia kupigia hela.huko huko UN...wanasingizia ili wapewe pesa ..

Unawaza kama mimi..
Hizo tafti sio kweli kabisa
 
Back
Top Bottom