Uniform za Polisi wa Kenya ni zipi haswa? Naombeni ufafanuzi

Christopher Wallace

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2015
Posts
1,479
Reaction score
3,788
Najua wanavaa blue lakini kwenye matukio mengi hasa hata ya kutangazwa kwa mshindi wa Urais wa Kenya hapo Bomas, naona askari wengi wamevaa kimbati za jeshi. Je nayo ni sehemu ya uniform za jeshi la polisi kenya?
 
[emoji23][emoji23][emoji23] sasa polisi ya kenya wavae hata kanzu ww unapata shida gani labda
 
kimbati kwa juu ni sehemu ya uniform za polisi wa kenya,lakini chini huvaa green kama wa kwetu tanzania.hao ni GSU ni kama FFU Tanzania.

wale wengine huvaa blue ambao ni sawa na wanaovaa khaki huku tanzania.
Na huyu mwenye rangi ya kaki ni jeshi gani?
 
Wale polisi wanaovaa nguo ya kijeshi (kijani) wametoka GSU. Wote ni polisi lakini GSU kazi yao ni extra security, more advanced. Wale ni para military police. Kazi yao ni kuzima moto wowote ule.

wale huitwa fanya fujo uone (FFU), na wana roho ya unyama na hawajalishi kama wewe ni mtoto, jibwa, mzee ama majaamzito wao watakuadhibu vilivyo.

Ole wako mkipatana na wao wrong place wrong time. Utatiii!!

πŸ˜‚πŸ˜­
 
Wale hawaibi mikate supamaketi
 
Najua wanavaa blue lakini kwenye matukio mengi hasa hata ya kutangazwa kwa mshindi wa Urais wa Kenya hapo Bomas, naona askari wengi wamevaa kimbati za jeshi. Je nayo ni sehemu ya uniform za jeshi la polisi kenya?
Kikatiba, Kenya inatambua askari wa Nation Police Service (NPS). Sasa NPS imegawanywa mara mbili:

1. Kenya Police Service. Hawa ndi wale huva sare aza blue



Chini ya KPS, pia Kuna GSU na DCI. GSU ni wa wakati wa fujo na pia hawa ndio hutoa ulinzi Kwa Rais na Makamu wake. DCI Mara nyingi hawavai Sare. Sare Mpya ya GSU hapa Chini



2. Kando na KPS, kuna Administration Police ambao huhusika na kazi tofauti



Ikumbukwe kwamba kuna sare tofauti depending on the function. Halafu pia, kuna sare nzee na mpya. Huko bomas, hakukuwa na Majeshi bali wote walikuw ni polisi waliotaka vikosi tofauti tofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…