"United States of Africa" na Ndoto za Bulicheka

"United States of Africa" na Ndoto za Bulicheka

Joined
Apr 8, 2023
Posts
30
Reaction score
23
Changamoto kubwa mbili zinazowakabili Waafrika kwa sasa katika ulimwengu, na kusema kweli zinazotunyima sauti kwenye majukwaa ya kidunia, ni Mamlaka (Sovereignty) na Nguvu za Kijeshi (Military Power).

Tuzungumze Mamlaka! Miaka 60 tangu kuundwa kwake, AU (African Union) imeshindwa kufikia maono ya (African United States) kwa sababu tu ya ubinafsi wa watawala wetu na hofu ya kupoteza "Uheshimiwa". Hofu hii ndiyo hasa inayotesa Waafrika siyo tu kwenye siasa, bali pia biashara na maisha yote kwa ujumla wake.

Leo Tanzania inao "matajiri" ambao wanaweza kuweka assets zao pamoja na kupata mtaji unaohitajika kuleta nchini Teknolojia ya kuchimba na kuchakata Madini yetu wenyewe, lakini hawako tayari kukaa pamoja. Kila mmoja anataka kuwa "Boss" wa "kidimbwi" chake mwenyewe akipiga kelele kwa nguvu hata anapomezwa na Tembo anayekausha maji ya kidimbwi chenyewe kwa funda moja. Ndivyo kwenye Siasa.

Leo AU haiwezi kusaini mikataba na pande nyingine za ulimwengu kwa ajili ya Afrika na Waafrika kwa sababu 'Wakuu' wa nchi ndiyo wenye Mamlaka na ndugu Faki na Mahamati wamebaki tu kuwa "highly celebrated clowns" wao. Hiki ni kichaa kibaya.

Mpaka Waafrika watakapokubali kujifunza kuheshimu uwezo maalumu kati ya ndugu zao, na kuutumia kwa faida ya Afrika, badala ya kila mmoja kutaka tu kuwa "mkubwa", hatutaona matokeo.

Pili ni nguvu za Kijeshi. Ni ajabu na kusema kweli kichekesho kwamba miaka 60 baada ya uhuru, bado Afrika inategemea majeshi ya kigeni kusaidia kutatua changamoto zake. Leo wakati Umoja wa Ulaya unatafuta njia ya kupeleka majeshi Ukraine, Waafrika wanategemea Navy Seals na Wagner Group kumaliza mgogoro (walioutengeneza wenyewe) wa Sudani. Hiki ni kichaa, tena kibaya kabisa.

Wakati Afrika ikijisifia kuwa na idadi kubwa ya watu wake walio vijana, tena chini ya miaka 35, unajiuliza wako wapi hawa vijana mbona hatuwaoni kwenda kuipigania na kuilinda Afrika!!? Najua mtaniambia operesheni za kijeshi ni aghali sana, na mimi nakubali, lakini Dhahabu, Almasi, Mafuta, Utalii na Chakula vilivyoko Afrika ndivyo vinavyolipia gharama za majeshi ya kigeni kwenye ardhi yetu na hivyo tatizo siyo fedha, ni uwezo wa fikra, mipango na utashi wa viongozi wetu, period!

Tanzania kwa mfano, ilikuwa na shule kadhaa zilizokuwa zikimilikiwa na kuendeshwa na jeshi letu ikiwamo Nyuki Sekondari na Air wing (sijui hali ikoje kwa sasa), na hilo lingeweza kusema kumbe ni rahisi kuwa na shule zenye mlengo wa kijeshi kuanzia msingi na kutengeneza viongozi imara na bora wa Kiafrika, lakini hilo halitokei kwa vile viongozi wetu wanaogopa "kupinduliwa".

Wakati nilipoona shule zinazoendeshwa na Guinea ya Mamady Doumbouya, nikajiuliza kwanini Afrika inao Majenerali wenye nguvu na waliofanya mageuzi makubwa kwenye mataifa yao, lakini hatuna shule za kijeshi kwa ajili ya watu hawa kitutengenezea falsafa za wanetu kabla hawajakwenda njia ya watu wote!!? Wote sisi badala ya kuwatazama watu kama Museveni, Obasanjo, Kagame, na wengine kutokea upande mzuri (maana kila mmoja wetu anao ubaya wake pia), tumekaza kuwatazama kama "Madikteta" tukidemkwa kwenye ngoma za watesi wetu na kupoteza fursa ya kujenga Jeshi la Afrika kwa ajili ya Waafrika.

Najua mnajua kwamba sijui lolote Nanga miye, hizi ni salaam tu nawasalimia!

1681833938774.jpg
 
Devide and rule, aliyekuwa anafanya juhudi za dhati za kuwaunganisha walimuua na kumuita dikteta(gadafi) na hakuna aliyeingilia, now haiatakuja kutokea hyo Muungano never
 
Back
Top Bottom