Mkuu kama unakumbuka Uingereza waliwahi kuanzisha maandamano wakiwa na madai kama ya South Africa, maajabu yake kwa swala lile lile ila kwakua ni Uingereza wakasema wanadai ajira zinazoweza kufanywa na wenyeji zibaki kwa wenyeji.
Miezi 2/ 3 nyuma kwa SA wakasema hiyo ni xenophobia.
- Ajira zinazoweza kufanywa na wenyeji, ni mantiki zibaki kwa wenyeji ilmradi wapo wenyeji ambao wana sifa za taaluma husika na hawana ajira.
- Hilo lipo dunia yote, leo hii ukienda kuuza mahindi choma Uchina, India n.k. utaona cha moto.
- Lakini ukienda na kuwa rubani, itaeleweka maana ni vigumu kupata marubani wazawa wasiokua na ajira.
- Hivyo kwa raia wa Uingereza kuandamana wakidai ajira kwa ajili ya wazawa, linaeleweka na kuwa na mantiki na tija.
- Sasa linakuja suala la sie Miafrika, unaandamana ili kufukuza Mwafrika mwenzio, hujali kama ni mtaalam wala nini.
- Unampiga Mwafrika mwenzio na kuwaacha wazungu na wahindi wakifanya kazi za kawaida tu.
Hata hapo kwenu Bongo, ipo siku niliingia kwenye ushindani na jamaa mzungu, ushindani wa kusaka mradi fulani, alinishinda kisa mzungu tu maana hakuwa na sifa sana zaidi ya ubabaishaji wa kuongea Kingereza kwa pua na kuwa na ngozi nyeupe.
Baadaye aliboronga nikaishia kuja mwenyewe kuifanya na kufanikisha hiyo kazi, Waafrika hatuaminiani, hatupendani, tunachukiana, na kuoneana wivu.....ukweli mchungu.