United states permanent resident card

AMOURY

Member
Joined
Aug 17, 2009
Posts
6
Reaction score
0
Hod humu ndani!
natumaini wote ni wazima kwa uwezo wa aliye juuu!(mola).
ni hivi waungwana, us department imenitumia e-mail kuwa nimechaguliwa kwenye hiyo permit tajwa hapo juu baada kufanyika random selection lakini pia niliwahi kujiunga kipindi falni maana wamenitumia ip adress ya compter yangu na tarehe niliyojiunga. mimi nilishasahau si mnajua mambo ya kusarf net.

SWALI LANGU SASA NI HIVI?
KWA WENYE UZOEFU HIKI KITU KIPO NA JE NI VALID AU NDO MAMBO YA KUTAKA KUNITAPELI? MAANA WAMESEMA INABIDI ULIPIE KAMA $440= Tsh 660,000/=
naomba kuwasilisha.
 
Fraud 419 hiy😵riginal Green Card alipiwi mkuu
 
Sidhani kama hiyo kitu ni ya kweli.Mara nyingi mawasiliano ya Permanent Residence/Green card huwa yanafanyika kwa njia ya posta.Kama uliwahi kucheza bahati nasibu yao yaani DV VISA Lottery na ukachaguliwa baada hiyo random selection utapokea barua/bahasha kubwa toka kwenye anuani yako ya posta ambayo ulijaza.

Kwenye hiyo bahasha kutakuwa na maelezo juu ya wewe kuchaguliwa na pia fomu za kawaida tu za VISA ya marekani.Utajaza hizo forms na kutakiwa kupiga picha na kuzituma kwenye address ambayo watakuwa wamekupa.Baada ya hapo watu huwa wanasubiri kwa muda wa miezi kadhaa mpaka watakapopata barua nyingine kwa njia ya posta inayokuarifu juu ya interview yako ya VISA,medical examination na mambo mengine unayohitaji kwa ajili ya kupata VISA yako.Hiyo card unayoizungumzia hapa huwa inatolewa wakati umeshafika US.Ukishawasili marekani huko ndo wanakutumia hiyo kadi kwenye address ambayo wewe utakuwa umeiandika kuwa utafikia.

So basically ni kitu cha namna hiyo.Huwa hakuna mawasiliano ya e-mail labda kama wewe utayaanzisha na local embassy au na watu wa immigration huko Marekani.
 
Matapeli hao mkuu green card inalipiwa fees kwenye Visa interview ambayo ni stage ya mwisho kabisa upewe visa na kuondoka. Tena fee yake ni$ 750 kwa mwaka jana ilikuwa. Halafu matokeo hayatolewi kwa email never, utatumiwa barua ya notification kwa adress yako. Halafu matokeo ya sasa yatatoka May 1 so kuanzia hapo ndo barua zitaanza kutumia

Kwa details zaidi nenda Electronic Diversity Visa Lottery utaona kila kitu na kujifunza process nzima

Ahsante
 
Du siku hizi hawa jamaa wanaua~yaani Visa $750 nakumbuka miaka ya 90's ilikuwa less than $300!.
 
Du siku hizi hawa jamaa wanaua~yaani Visa $750 nakumbuka miaka ya 90's ilikuwa less than $300!.

Yah wanaua sn siku hizi hapa bado hujafanya medical exams mzee ujipange kwa airticket tena du inabidi ujipange. Halafu Visa wanatoa ya 6 Months only uwe ushaingia US!
 

Hiyo fedha ni ya fomu gani? Na sender ametuma kutokea department of state? Lazima email yake iishie na .GOV. Zaidi ya hapo, huwa hawombi fedha.
Check from their website DV 2011 results and see if you are in.

2011 Entrant Status Check

Please click this link http://www.dvlottery.state.gov/ESC/ for DV-2011 Entrant Status Check.
 
Hao ni wezi tu, hela uitume wapi sasa?
Nenda kwenmye hiyo link cheki kama umeingia na pia inabidi ujiandikishe kila mwaka for lottery so kama hukujiandikisha ya 2011 hauwezi ukawa umeshinda.
 
Nawashukuru sana ndugu zangu nimesoma maelezo yote kwenye website yao,jamaa walitaka kunitia damage ya ukweli, kulingana na maelezo yao na vigezo vyao mpaka wakuchague inabidi uwe umejaza form kitu ambacho sikuwai kufanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…