Ukweli ni kwamba UDSM haipo kulingana na umri wake
kama chuo cha kwanza nchini, yeyote angetegemea Graduate wa pale awe special, ( academic character) Hilo halina ubishi. ukizingatia kuwa Chuo hicho kitakuwa na walimu waliofaulu (mmoja/waiwili wakti huo hamna kata SS) waliopata point nzuri form four,( wakati huo A_level chache) wakaenda form six by then, generally vipanga. hivyo output itakuwa ya juu sana. Sijui mawazo ya mtoa mada, but Point ni kwamba tunategemea tukisoma habari gazetini nzuri huyo mwandishi kasoma udsm, daktari bingwa kasoma udsm, nk. kwa maneno mengine UDSM kwa leo kama kila baada ya mwaka ingekuwa inaanzisha kozi leo ingekuwa na degree 50 au zaidi inatoa, na kwa wanafunzi wazuri tu. ( wenye uwezo wa juu kiakili)
Pili, mtu yeyote anategemea kuona tofauti ya graduate wa UDSM na SAUT, St James, IFM, Mbeya tech, Morogoro Muslim, st Gasper, Theophil k, nk. hii tofauti haijalishi waandishi, engineers, economists etc ila UDSM graduate apate kuwa na tofauti na other universities.
Pengine tunatumia fananishi ya dunia ya kwanza, kama umegraduate Yale, Cambridge, Havard lazima tukuangalie kwa macho mawili, na ukiongea tukusikilize. Je leo Graduate wa UDSM wana hizo sifa?
Mwisho, najua kuna makosa, au makusudi, yalifanyika kuiondoa UCLAS, MUCHS etc, sababu chuo kikubwa kama hicho lazima kiwe na school za kutosha na degree nyingi kupita maelezo, na graduate wake wawe tofauti na vyuo vingine.
wakatabahu.