Unleashed: Vol-1 - P-X:2010 - "Fikra mbadala"

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Unleashed – Vol. 1 “Fikira tofauti za mabadiliko” ni mfululizo wa makala sita (moja ni ya Rev. Kishoka) ambazo zote zina lengo la kuzidi kuchochea mabadiliko ya fikra ambayo hutangulia mabadiliko ya kura. Makala hizi zote zinaweza kuchapwa na gazeti lolote la Tanzania bila kubadili maudhui yake au jina la mtunzi. Makala zote zinapotumika kwenye magazeti zihakikishe zinabakia jina la Mtunzi na vile vile kutoa anuani ya barua pepe iliyo chini ya kila makala.


  • Alichosema Mwakyembe ndiyo kauli ya Vita
Katika makala hii ninaangalia kauli iliyonukuliwa na gazeti la MwanaHalisi kuhusu Dr. Mwakyembe katika mgongano uliotokea kwenye kikao cha NEC kule Dodoma wiki chache zilizopita. Kauli hiyo tukiifuatilia ninaamini inatosha kabisa kuwa ni mbiu ya mapambano haya ya kuutokomeza ufisadi. Katika hili, wapambanaji CCM wamechukua msimamo sahihi na wa kuungwa mkono.


  • Kuulewa mfumo wa Utawala wa Kifisadi (MUK) – 207
Hii ni mwendelezo wa makala ya kuelewa mfumo wa utawala wa kifisadi. Hii ni kozi nzito na mada nzito ambayo inahitaji uvutaji pumzi wa mara kwa mara kuweza kuzama. Hii siyo mada kwa watu wavivu kusoma au kufikiri au wanaochoka mapema kuchambua mambo. Kama ulielewa sehemu ya 101 basi uko tayari kuendelea mbele. Katika makala hii tunaangalia wanufaika, waathirika, na wanusurika wa mfumo wa kifisadi.


  • Na Wapo Machangudoa wa Ufisadi
Baada ya kuingiza maneno ya “watawala wetu”, “Makuwadi wa ufisadi”, “vikaragosi vya ufisadi” naomba niongeze neno jipya katika misamiati hii ya vita; kuwa wapo pia “machangudoa wa ufisadi”. Hawa ni wengi na wengine wapo miongoni mwetu. Makala hii ina lugha na picha za mafumbo zenye kugusa watu wazima. Soma kwa kukereka kwako.


  • Tuache kumsingizia Mungu, tujiandae kwa majanga
Hii ni mwendelezo wa makala mbili nilizotoa mwaka jana. Moja mwezi Aprili na nyingine baada ya vifo Tabora Oktoba Mosi mwaka jana. Oktoba mosi imekuja wiki iliyopita bila ya watu hata kukumbuka siku ile ya huzuni. Ni makala ambayo pia imetokana na kufuatilia vifo vya watoto wengine katika ajali ya moto wiki hii iliyopita. Ni makala yamapendekezo ya kina ya kujiandaa kwa majanga. Mtu yeyote ambaye ni kiongozi wa ofisi, idara, wizara au kitengo fulani ningemlazimisha kuisoma.


  • Usalama wa Taifa lazima ubadlike, kama tunataka tusalimike
Hii ni sehemu ya kwanza ya makala ya mapendekezo yamabadiliko yanayohitajika katika idara ya Usalama wa Taifa. Makala hii imekuja baada ya kuombwa kwa muda mrefu na baadhi ya marafiki zangu wa idara hii kuandika juu ya hali ya usalama wa taifa nchini. Nilivunja mwiko wa kuijadili idara hii mwaka jana na Zitto akavunja Mwiko Bungeni mwaka huo huo, na sasa naona tuende mbele zaidi. Kama sehemu ya kwanza, ni kozi tosha kabisa kwa mtu anayetaka kuelewa usalama wetu wa taifa umetoka wapi na unaelekea wapi.

  • Ukahaba wetu unatuponza
Makala hii ni ya Rev. Kishoka ambayo tukiwa tumeandika nyakati tofauti na bila ya mawasiliano tumejikuta tukigusia kitu kile kile. Nimemuomba niambatanishe kwenye mfululizo huu. Nayo kama hiyo ya kwangu ya “machangudo” nayo imejaa picha na hoja za nguvu. Kwa mara nyingine, Mchungaji wetu anazidi kuvutia kwa utamu wa maandishi yake.



NB: Unaweza kuangalia moja moja kama zilivyohapa au kuzichukua kama sanduku moja la .RAR na ukalifungue kujisomea kwa raha zako. Ukiweza sambaza kwa wale wanaoweza kuzisoma!

Katika volume ya pili mojawapo ya mada nilizozifanyia kazi kwa muda mrefu ni ile ya "UKOSOAJI WA WAZI WA CHADEMA - 1).
 

Attachments

Last edited by a moderator:
Mkuu safi sanaaaa!
Sasa ukisikia waraka basi huu ndio WARAKA!
Pongezi mkuu wangu, kazi kubwaumeifanya...
 
Mkuu safi sanaaaa!
Sasa ukisikia waraka basi huu ndio WARAKA!
Pongezi mkuu wangu, kazi kubwaumeifanya...

Asante mkuu; tuko pamoja! Nakusoma sana mkuu japo sipati muda kama wa zamani kuchangia sana. So, imebakia kuja na volumes tu! kwi kwi kwi..!
 
Mwanakijiji unajua sana kuweka facts sawasawa; nimefurahia sana ulivyozipangilia kinyume na wao wanaohubiri sehemu ndogo inayowafurahisha tu na kuacha picha kubwa ya mambo yenyewe,

Hongera sana na Mungu akuzidishie nguvu za kuendelea kuielimisha jamii yetu inayosahau mambo haraka haraka.
 

Mkuu haya maneno yako ni mazuri mno na yamekuja wakati muafaka. Tuna hiari ya kuyasikiliza au kuyadharau. Kama tutaamua kuyadharau, it would be at our own peril.Mabadiliko ni kitu muhimu sana kwa sababu hata kama hatutaki kubadilika, mambo yanayotuzunguka yanabadilika kwa kasi na tutakaopoteza ni sisi. UWT wanajua wazi hilo maana hata namna ya kukusanya habari za kijasusi leo sio sawa na juzi. People have become more sophisticated as a result of technological evolution.

Namalizia kwa maneno ya Charles Darwin kuhusu umuhimu wa kuwa flexible na changes.

It is not the strongest of the species that survives, nor the most intelligent that survives. It is the one that is the most adaptable to change.

Naunga mkono hoja ya kuzibadili system zetu jinsi zinavyofanya kazi ili ziende na wakati na kuwa na resources zinazomudu mahitaji ya sasa kwa manufaa ya siku zijazo. Mungu ibariki Tanzania!
 
Mwanakijiji na Rev Kishoka, big up kwa kazi mnayofanya Mungu atawasaidia na kuwalinda!
 
Asante Mzee wangu Mwanakijiji!! naona umekuja kutupa na kufanya yale ambayo kwa miezi kadhaa ulikuwa unayafanya, sasa tumekuelewa ubarikiwe mzee wangu
 
You are really smart guy.. I will pray for you Babu yangu na Mungu akusaidie bwana
 
Asante Mwanakijiji; ila mimi mbona kama naona makala tano tu? Sijaiona hiyo ya Rev. Kishoka. Labda ni IT inanigonga?
 
Juhudi zako ni nzuri na muhimu lakini tatizo ni watu kuelewa ni nini hasa unacho kiongea na kutekeleza. Mengi Mwanakijiji umesema na kuandika lakini nikitazama tunayafanyia kazi vipi na wapi sioni, wengi tumedhoofika na madhara ya ufisadi nakujiona ni sehemu ya machangudoa wa ufisadi.
 
Samahani. Makala ya Kishoka iko kwenye hilo file la rar.
 
Kudos to you Mzee Mwanakijiji na Rev Kishoka
 
Mkuu mwanakijiji na kushoka mpo juu jamani.Articles zenu zipo well organized na endapo zitatiliwa maanani then nchi hii itabadilika, mbarikiwe sana na big up all!!!
 

Tunajaribu na kuchangia kidogo tulichonacho kwenye bahari ya fikra tele; chetu ni chembe moja ya mchanga na ni cheche moja ya moto~!
 
Mwanakijiji na Rev Kishoka, big up kwa kazi mnayofanya Mungu atawasaidia na kuwalinda!

ndugu yangu; shetani akikupania wakati mwingine unajiulliza kama Mungu yuko upande wako; saa ya mjaribu yaja.
 
Asante Mwanakijiji; ila mimi mbona kama naona makala tano tu? Sijaiona hiyo ya Rev. Kishoka. Labda ni IT inanigonga?

ya Kishoka sasa imeongezwa naona mara ya kwanza sikuibandika hata kwenye sanduku la rar lenye mafaili mengine matano.
 

Kuna kizazi kitakuja kuyafanyia kazi haya; lakini pia sisi wengine tumedokeza mambol ambayo tutayafanyia kazi tutakaposhika madaraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…