'Unlimited Jurisdiction' of The High Court

'Unlimited Jurisdiction' of The High Court

Malengo Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2013
Posts
287
Reaction score
99
2. JURISDICTION OF THE HIGH COURT
OF TANZANIA.
"The Court has unlimited Jurisdiction on
both Civil and Criminal matters within
Tanzania. In addition to the said original
and jurisdiction, the High Court of
Tanzania has an appellate, extended,
revision and supervisory jurisdiction over
subordinate Courts.
Appeals from the High Court are
preferred to the Court of Appeal of
Tanzania which is vested with powers,
authority and jurisdiction of confirming,
reversing or varying any decision made by
the High Court."

Nimeanza kwa quotation toka tovuti ya mahakama kuu just to make my self clear. Kwa maelezo hayo hapo juu na kwa jinsi nilivyofundishwa na lecturer wangu, The High Court has 'unlimited jurisdiction' i.e it has powers & authority to exercise or entertain any matter of any kind, value, nature n.k hapa Tanzania.

Swali langu ni pale ninaposoma baadhi ya hukumu za Mahakama Kuu ya Tanzania na kukuta maamuzi yanayosema "This court has no jurisdiction because the matter in question is political"

Kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba Mahakama kuu kwa sasa imecreate exception to the general rule that The High Court has unlimited jurisdiction" Lakini nkitazama katiba yetu ya 1977 inaniambia Mahakama ndio chombo cha mwisho cha utoaji haki katika nchi hii. Je wanaokosa haki katika siasa wakaitafte wapi kama mahakama imejivua wajibu huo?

Wadau nyie mnafikiri haya maamuzi ya Mahakama ni Sahihi? Je kama mahakama haina mamlaka ya kuamua mambo ya wanasiasa je ni sahihi kuamua mambo ya wafanyabiashara, wakulima na wafanyakazi? (High court commercial, land and labour division respectively).

Mchango wako please!!
 
Hiyo ndio reference itakayokuwa ikifanyika kwenye mahakama nyingine huko duniani kuwa "hukumu hii ilitolewa na nchi huru mwaka 2014".
Ukiwa na nchi yenye wanasheria, madaktari, wahasibu nk wa aina hii huwezi kuvumbua hata pini ya kutolea funza!
 
Je mambo yakienda mrama kwenye siasa watu wakaenda mahakamani na mahakama nayo ikajivua mamlaka ya kutoa uamuzi, je watu wakizitafta haki hizo kwa njia zisizo halali wala kisheria watalaumiwa kwa lipi?
 
Mtoa mada nashukuru kuwa umeiweka mada hiyo vizuri kwa kuweka bayana mamlaka ya mahakama kuu nchini Tanzania na na mambo ambayo mahaka hiyo ina mamlaka nayo ya kuyasikiliza na kuyatolea maamuzi.

Ni kweli kuwa baadhi ya majaji wa mahakama kuu wamevua madaraka ya mamlaka hiyo kwa kuangalia maslahi yao zaidi sana kujenga mahusiano ya kuwafurahisha wanasiasa. Jambo kama hilo ni la aibu kwa chombo hicho cha kutafsiri sheria za nchi na kutoa haki katika taifa hili. Ni jambo la fedheha kubwa kusikia maneno kama hayo kuwa eti jambo hili ni la kisiasa zaidi. Kwa hiyo haki inapominywa katika uwanja wa kisiasa na mahakama imejivua wajibu wa kutoa haki katika eneo hilo basi itafsiriwe kuwa kwenye siasa fujo ni halali. Inakuwaje sasa mahama hiyo hiyo inasikiliza malalamiko ya wanasiasa wanaposhindwa kwenye chaguzi? Je uchaguzi siyo suala la kisiasa hilo? Nadhani wasomi wetu katika nyanja hii wanaitia kitanzi mahama kwa kuoiondolea mamlaka iliyonayo na ambayo katiba ya nchi iliipa. Majaji wa namna hiyo wanapaswa kujitadhmini kama wanastahili kuendelea katika nyadhifa zao.
 
Mkuu nakupa like kwa uchambuzi wako na naomba niongezee kuwa hawa majaji kama wanaona hukumu zao ni sahihi na kwamba wanastahili kuendelea kushika nyadhifa zao, basi ni vema na katika hukumu za namna hiyo pia wawe wanaeleza haki zilizokosekana katika uwanja wa siasa wanaozidai mahakama iwaoneshe sehemu ya kuzipata kama yenyewe haiwezi kuzitoa.
 
Back
Top Bottom