Unrwa yapigwa marufuku na bunge la Israel

Digaller

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2009
Posts
798
Reaction score
541
Bunge la Israel limepiga kura kupitisha sheria ya kupiga marufuku shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina (Unrwa) kufanya kazi ndani ya Israel na Jerusalem Mashariki inayokaliwa na Israel, ndani ya miezi mitatu.

Mawasiliano kati ya wafanyakazi wa Unrwa na maafisa wa Israel pia yatapigwa marufuku, na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa uwezo wa shirika hilo kufanya kazi huko Gaza na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel.

Ushirikiano na jeshi la Israel, ambalo linadhibiti vivuko vyote vya Gaza ni muhimu kwa Unrwa kuhamishia misaada katika eneo lenye vita. Ni shirika kuu la Umoja wa Mataifa linalofanya kazi huko.
Wafanyakazi wa Unrwa hawatakuwa tena na kinga ya kisheria ndani ya Israel, na makao makuu ya shirika hilo huko Jerusalem Mashariki yatafungwa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alisema kutekeleza sheria hizo "kutakuwa na madhara kwa utatuzi wa mzozo wa Israel na Palestina na kwa amani na usalama katika eneo kwa ujumla", huku mkuu wa Unrwa Philippe Lazzarini akisema "itazidisha mateso ya Wapalestina."

Nchi kadhaa, zikiwemo Marekani, Uingereza na Ujerumani, zimeelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu hatua hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Lammy aliiita "makosa kabisa", wakati Waziri Mkuu Sir Keir Starmer alisema sheria zinahatarisha kufanya "kazi muhimu ya Unrwa kwa Wapalestina isiwezekane, na kuhatarisha mwitikio mzima wa kibinadamu wa kimataifa huko Gaza".

Source: BBC Swahili

Source: Israel yapiga marufuku shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina - BBC News Swahili
 
unrwa ni magaidi tupu mle....yafagililiwe tu chap..usafi wa kina uendelee pale gaza
FB_IMG_1730173617571.jpg
 
Baadhi ya wafanyakazi wa UNRWA ni wanachama wa makundi ya kigaidi ndio maana Israel imechukua hatua kali kufungia hiyo NGO uchwara.
Safi sana
Kuna uzi. Mdau aliuleta humu
 
Bunge la Israel limepiga kura kupitisha sheria ya kupiga marufuku shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina (Unrwa) kufanya kazi ndani ya Israel na Jerusalem Mashariki inayokaliwa na Israel, ndani ya miezi mitatu.

Mawasiliano kati ya wafanyakazi wa Unrwa na maafisa wa Israel pia yatapigwa marufuku, na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa uwezo wa shirika hilo kufanya kazi huko Gaza na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel.

Ushirikiano na jeshi la Israel, ambalo linadhibiti vivuko vyote vya Gaza ni muhimu kwa Unrwa kuhamishia misaada katika eneo lenye vita. Ni shirika kuu la Umoja wa Mataifa linalofanya kazi huko.
Wafanyakazi wa Unrwa hawatakuwa tena na kinga ya kisheria ndani ya Israel, na makao makuu ya shirika hilo huko Jerusalem Mashariki yatafungwa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alisema kutekeleza sheria hizo "kutakuwa na madhara kwa utatuzi wa mzozo wa Israel na Palestina na kwa amani na usalama katika eneo kwa ujumla", huku mkuu wa Unrwa Philippe Lazzarini akisema "itazidisha mateso ya Wapalestina."

Nchi kadhaa, zikiwemo Marekani, Uingereza na Ujerumani, zimeelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu hatua hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Lammy aliiita "makosa kabisa", wakati Waziri Mkuu Sir Keir Starmer alisema sheria zinahatarisha kufanya "kazi muhimu ya Unrwa kwa Wapalestina isiwezekane, na kuhatarisha mwitikio mzima wa kibinadamu wa kimataifa huko Gaza".

Source: BBC Swahili

Source: Israel yapiga marufuku shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina - BBC News Swahili
West kama kawaida yao wasiwasi wake mkubwa...
 
Back
Top Bottom