You still haven't shown how English is a benefit of colonization. Kwani nchi ambazo haziku tawaliwa na Britain hawana watu wanao ongea Kingereza? My point still remains how is it a benefit from colonization if we didn't have to be colonized to speak it? Kwani wote wanaongelea kingereza wame tawaliwa na wakoloni? Na imetu benefit vipi wakati even the majority of Tanzanians don't even speak it? Na hizo other benefits zitaje basi si zipo nyingi kama unavyo sema?
Okay, haya twende taratibu.
Wakoloni walijenga miundombinu ambayo hadi hivi leo bado tunaitumia. Tuanzie na reli ya kati. Ndio, labda dhumuni la wao kujenga hiyo reli ilikuwa ni kurahisisha usafirishaji wa mazao n.k. Lakini baada ya wao kuondoka hawakuzing'oa hizo reli. Walituachia na sisi tukazipokea na kuendelea kuzitumia.
Nimepanda sana treni mimi ya kwenda Mwanza na kushukia Shinyanga. Enzi hizo usafiri wa basi ulikuwa mgumu kweli. Kulikuwa hakuna njia ya kuaminika kwenda hiyo mikoa ya kanda ya ziwa. Usafiri wa ndege sio kila mtu alikuwa anaweza kumudu. Sasa uje wewe unambie eti mimi sijafaidika na kuwepo kwa reli ya kati kwa kweli nitakushangaa.
Kuna wafanya biashara wengi sana wa kutoka mikoa ya kanda ya ziwa waliokuwa na bado ambao wanatumia hiyo reli kusafirisha bidhaa zao kuleta Dar-es-Salaam na mikoa mingine. Unataka kunambia hawafaidiki kuwepo na hiyo reli? Mwambie babu yangu na wajomba zangu waliokuwa wanasafirisha ng'ombe wao kutoka Mwanza na Shinyanga kwenda Kibaha kuwa hiyo reli haina faida yoyote uone kama watakuelewa.
Kuna shule ngapi ambazo wakoloni walizijenga na walipoondoka hawakuzivunja? Ni viongozi wetu wangapi ambao wamepitia ktk hizo shule? Ni wasomi wangapi ambao tunao leo tunaojivunia ambao wamepitia shule zilizojengwa na mkoloni?
Bandari yetu ya salama tuliyonayo leo hii tumeijenga wenyewe? Ni nchi ngapi zinazotumia bandari yetu? Kama kila kitu cha wakoloni kilikuwa kibaya basi tungeibomolea mbali na kujenga upya.
Nenda Oysterbay, Upanga na kwingineko uhesabu ni nyumba ngapi zilizojengwa na kuachwa wakoloni ambazo wanaishi Watanzania sasa hivi. Kwa nini baada ya uhuru hatukuzivunja na kujenga za kwetu wenyewe?
Ni Watanzania wangapi wanaoenda kutibiwa pale hospitali ya Ocean Road? Umewahi kufika kwenye hiyo hospitali wewe? Hiyo hospitali imejengwa na mkoloni na leo hii ndio taasisi kubwa Tanzania inayotibu magonjwa ya saratani. Nenda kawaambie wagonjwa wote wanaotibiwa hapo kuwa hiyo hospitali haina faida yoyote kwao kwa sababu ilijengwa na wakoloni.
Mimi sikatai kuwa ukoloni ulitunyima haki yetu kubwa ya msingi ambayo ni uhuru na uwezo wa kujitawala na kujiamulia mambo yetu wenyewe. Lakini vilevile nitakuwa si mkweli nikikataa katakata kuwa ukoloni haukuleta faida zozote zile. Malengo na madhumuni ya wakoloni kujenga makoloni yao pengine yalikuwa ni ya kuwanufaisha wao zaidi lakini vilevile na sisi waliotuachia tumenufaika na tunaendelea kunufaika pia. Tungeona kuwa vyote walivyotuachia havina faida yoyote basi baada ya wao kuondoka tungeondokana navyo vyote.
Kuna raisi mmoja huko Afrika Magharibi, Sekou Toure wa Guinea kama sijakosea ambaye aling'oa hadi milingoti ya taa za umeme za barabarani baada ya Wafaransa kuondoka na baadaye kujikuta anaomba msaada wa vile vile alivyovibomoa kutoka kwa rafiki yake Kwame Nkrumah. Now how smart was that?