Ununuzi wa kiwanja

Ununuzi wa kiwanja

siriusblack

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2013
Posts
218
Reaction score
301
Habari zenu wakuu

Kuna mtu anauza kiwanja ambacho hakijapimwa maeneo ya Kigamboni eneo la muongozo - Shirikisho
Tatizo langu kubwa ni kwamba sina jinsi/namna ya kumjua muuzaji au mmiliki halali wa eneo hilo - nilienda mpaka serikali za mitaa na nikakutana na mwenyekiti na amenihakikishia kwamba hao ndo wauzaji halali wa hilo eneo

Hivi katika mazingira kama hayo kwa watu wazoefu wa masuala ya mauziano ya viwanja naweza kuchukua hatua gani zaidi ili nisije kupata matatizo baadaye pamoja na kwamba office ya serikali ya mtaa imehusika

Nahitaji uzoefu kwenye hilo suala
 
mwambie anayekuuzia mke wake mtoto wa kiume na ndugu yake mmoja awepo
 
Habari zenu wakuu

Kuna mtu anauza kiwanja ambacho hakijapimwa maeneo ya Kigamboni eneo la muongozo - Shirikisho
Tatizo langu kubwa ni kwamba sina jinsi/namna ya kumjua muuzaji au mmiliki halali wa eneo hilo - nilienda mpaka serikali za mitaa na nikakutana na mwenyekiti na amenihakikishia kwamba hao ndo wauzaji halali wa hilo eneo

Hivi katika mazingira kama hayo kwa watu wazoefu wa masuala ya mauziano ya viwanja naweza kuchukua hatua gani zaidi ili nisije kupata matatizo baadaye pamoja na kwamba office ya serikali ya mtaa imehusika

Nahitaji uzoefu kwenye hilo suala
Uliza majirani pia kuhusu nani ni mmiliki wa kiwanja hicho, viwanja vingine vina migogoro utajikuta unanunua mgogoro
 
Usilipie mpk uonane na majirani wa pande zote nne za kiwanja. Pia rudi peke yako kwenye eneo ulizia mmiliki wake na majirani wa muda mrefu wa hilo eneo utapata jibu
 
Back
Top Bottom