Kitchen party haiwezi kuwa na maana kwa vile ni kitu cha siku moja tu, unless awe bibi harusi mtarajiwa aliwekwa ndani kwa muda. Mafunzo hayo kama nilivyosema kikwetu hayakuwa ya muda mfupi hivyo. Ukishazaliwa tu vibibi vikishangilia ni "msichana!" unaanza mafunzo hapo hapo kulingana na umri, mafunzo ya mambo mengi sana sana. Hadi unapopata mchumba hata kiuno ni laini kuzungusha kwa vile utakuwa umeanza mazoezi ya kunengua taratibu kadri unavyokua, mnapokwenda kutafuta kuni, mnapokwenda visimani, mnapocheza wenyewe, mausia ya wamama wakubwa, jinsi ya kuketi kama msichana sio kutanua miguu ka dume. Mzungu alipokuja akasema ni ushenzi, vikatupiliwa mbali, matokeo yake ndo hayo, balaa tupu haijulikani nani HE nani SHE ndani ya nyumba. Mafunzo hayo yalikuwa na bado ni muhimu. Yoooteee kumhusu mama kama mwanamke yalifundishwa kulingana na umri wa mtoto wa kike. Ati leo yanafundishwa kwa masaa??? Mwe! Utaelewa nini? Matokeo kiuno kigumu ka milingoti ya reli, hujui hata kupakata watoto, huelewi mume ndio nini, hujui usafi wala heshima wala hofu ya Mungu. We haya weeee!