Unyakuo ni nini? Je, watakaoachwa duniani baada ya unyakuo, watapatwa na nini?

Unyakuo ni nini? Je, watakaoachwa duniani baada ya unyakuo, watapatwa na nini?

Unyakuo ni tafsiri ya Kiswahili ya neno la Kiingereza "rapture."
Unyakuo ni tukio litakalotokea siku Yesu atakapokuja kuwachukua watakatifu, yaani watu waliookoka, na kuwapeleka mbinguni. Ni tukio litakalofanyika ghafla(kufumba na kufumbua)!

Maana itatolewa amri, sauti ya malaika mkuu, sauti ya tarumbeta ya Mungu, naye Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni. Ndipo wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai wakati huo tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu kumlaki Bwana hewani..."(1 Wathesalonike 4:16-17)

Itakuwaje sasa au kutatokea nini kwa watu watakaoachwa duniani baada ya unyakuo?

Haya hapa ni baadhi ya mambo yatakayotokea duniani kulingana na Maandiko:

1. Dhiki kuu
Mara baada ya unyakuo, dunia itaingia katika kipindi cha dhiki, giza na mateso kisicho na mfano – kinachoitwa Dhiki Kuu (Great Tribulation).

Mathayo 24:21
"Kwa kuwa wakati huo kutakuwa na dhiki kuu, ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa..."

Wale watakaobaki duniani baada ya unyakuo, watakumbana na vurugu, vita, magonjwa mazito, njaa, na hofu kubwa. Hakutakuwa na utulivu kabisa. Dunia itakuwa katika hali ya kiwewe na machafuko makubwa ya kiroho na kijamii.

2. Utawala wa Mpinga Kristo
Mpinga Kristo atainuka kama kiongozi wa dunia, mwenye nguvu na ushawishi mkubwa. Ataonekana kuwa mleta amani mwanzoni, lakini baadaye atageuka kuwa mtesaji mkubwa wa waliobaki (2 Wathesalonike 2:3-4).

Atawalazimisha watu wamsujudie. Watakaokataa kumsujudia au kuchukua chapa yake (alama ya 666), watateswa sana na kuuawa.

3. Alama ya 666 itatolewa kwa nguvu
Hakuna mtu atakayeruhusiwa kununua au kuuza bila kuchukua alama ya mnyama – chapa 666.

Ufunuo 13:16-17
"Naye awalazimisha wote… watiwe chapa katika mkono wao wa kuume au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa hiyo…"

Watakaochukua alama hiyo watakuwa wamemtii shetani, hivyo watahukumiwa kwenda motoni milele.

4. Mapigo mazito yatamiminwa duniani
Mfululizo wa mapigo saba mazito yataachiliwa juu ya dunia kama hukumu ya Mungu.

Ufunuo 16:1
"Nikasikia sauti kubwa kutoka hekaluni ikiwaambia wale malaika saba: Nendeni mkamwage vikombe saba vya ghadhabu ya Mungu juu ya nchi."

Hakutakuwa na kimbilio. Dunia itakumbwa na mateso ambayo haijawahi kushuhudia.

Ndugu zangu, tugeuke, tubadilike, wakati huu ambapo neema bado haijafungwa.

2 Wakorintho 6:2
"...Tazama, wakati uliokubalika ndio huu, siku ya wokovu ndiyo hii."
Uongo, hii ni tafsiri potofu.
 
SIJUI MAMBO YA SIASA WALA VITA NA SIFAUTILII

NINACHOJUA YESU AMESHUHUDIA KWA UFUNUO KUWA.
NCHI YA IRANI INAMILIKI SILAHA AMBAZO HAKUNA NCHI YEYOTE DINIANI YENYE NAZO

AMBAZO HATARI ZAIDI DUNIANI ZENYE UWEZO WA UHARIBIFU MKUBWA ZAIDI KWA SEHEMU KUBWA YA DUNIA HII

AMBAPO YESU AMESEMA
HATARUHUSU NCHI YA IRANI IZITUMIE SILAHA HIZI HATARI ZAIDI DUNIANI
KABLA HAJANYAKUA WATAKATIFU

WAKE WALIOPO HAI HAPA DUNIANI

HIZO ZITATUMIKA BAADA YA UNYAKUO(LABDA).

UNYAAKUO WA KANISA (WATAKATIFU WALIOPO DUNIANI)UTATOKEA KABLA YA 2030.

ni kama ndani ya miaka hii 2-3 ..muda umeshafika

Mtakatifu na azidi kutakaswa,tuyafue mavazi yetu yawe meupe.
 
Back
Top Bottom