Mimi nadhani huyu mkuu ni mchunganji na anatafuta nafasi ya kuhubiri. Sina tatizo kuhubiriwa. Ni vyema. Baadaye itapita kapu tuchangie. Sina shida kuchangia, ni vyema. Roho mtakatifu amempotezea njia ili aje hapa jukwaa la biashara apate mawaidha kuusu kanisa vs pesa. Kwanza ni vizuri makanisa yaanze kulipa kodi ya mapato wanayo kusanya makanisani kama sadaka - Hii itatimiza vile ilivyo andikwa 'Ya kaisari mpe kaisari na ya Mungu mpe Mungu (mark 12:17, mathew 22:21) na pia watoe receipt kutoka kwa ETR - Electronic Tax Register- kwa kila muhumini aliye changia. Ni muhimu pia kuwe na tume maalum ya kuhakikisha kanisa haliendeshwi kama mali ya mtu binafsi. Hii itatuondolea makanisa yanayo undwa na watu wenye malengo ya kupata pesa tu. Wanawaweka wake zao, waume zao kama directors wa kanisa na mwisho wake wanaacha uridhi wa mali ya kanisa kwa wanawe wakati kanisa ni mali ya waumini wengi. Biblia inatutangazia kwamba siku za mwisho watakuja watakao tuhubiria uongo. Kuepusha hii kitu inabidi kuwe na bodi za wakristo zenye uwezo wa kumtoa muhubiri anaye fundisha kitu ambacho hakiendani na biblia au anaye tumia mali za kanisa vibaya, kisa na maana kuwa ndiye mwanzilishi wa hilo kanisa. Mambo haya yapo zaidi kwenye makanisa ya watu binafsi sio mainstream churches. Moja wapo ya majukumu ya kanisa ni kusaidiana na serekali kuondoa umasikini, tume liwe linapata feedback ni vipi kanisa linafanya hili. Baadaye nadhani tuzungumzie gharama za unyakuo, watakao pata faida kwenye unyakuo tuwajue na watakao pata hasara, ili tujipange mapema. Tutakao baki tujue kama tunaweza kuzamia nchi za waarabu ambao labda hawatanyakuliwa. Karibu sana kwenye jukwaa la biashara mkuu, utuongezee ufahamu kuusu haya mambo