Unyama aliofanyiwa mtoto huyu ulaaniwe

Unyama aliofanyiwa mtoto huyu ulaaniwe

Boran Jakutay

Senior Member
Joined
Apr 8, 2023
Posts
110
Reaction score
259
Screenshot_20230423-172355.jpg

Binadamu baadhi yetu wana wivu, chuki na roho mbaya inayowafanya kutumia njia zozote kuhakikisha jambo lao baya linafanikiwa.

Soma alichokisema mtoto huyu ambaye ni msanii kutoka Congo namna alivyopata upofu wakati alizaliwa akiwa anaona vizuri.

"Mimi sikuzaliwa kipofu, nilizaliwa naona kama watoto wengine lakini kwa sababu ya kipaji changu alikuja mama mmoja na nguo nyeusi akanifuta nayo uso na kuanzia hapo nikapoteza uwezo wa kuona.

"Kwa sasa nimepata miwani ambayo ninaitumia inanisaidia kuona" - MC Baby mwimbaji kutoka Congo.

Chanzo: Clouds Media
 
Kuna na mwingine alijifungua jiwe kimaskhara maskhara
 
Kuna asiyeona mmoja alipata kunisimulia mwaka 2004, anasema walikuwa katika mazingira ya kazi kama kawaida (yeye alikuwa dereva).
Katika stori, mwenzake akamuuliza, kati ya kufa na kutokuona unachagua nini? Akajibu heri kutokuona.
Kuanzia siku ya pili hakuona tena.

Hii dunia ina vitu vya ajabu sana japo vingine ni ngumu kuvithibitisha.
 
Back
Top Bottom