abelkiharo
New Member
- Aug 27, 2022
- 2
- 1
Huenda likawa jambo gumu kwako kuamini, lakini ukweli ni kwamba; kiwango cha unyanyasaji kwa wajawaito katika maeneo ya kutolea huduma za afya ni kikubwa sana. Ni jambo linalosikitisha, kuona wale watu ambao jamii imewaamini kwa ajili ya kunusuru maisha ya wengine, ndio hao ambao wanaendelea kufanya vitendo ambavyo ni kinyume na ubinadamu!
Tafiti zinaonyesha kwamba wajawazito wengi hujifungulia nyumbani kwasababu ya kukwepa manyanyaso ya wataalamu wa afya kutoka katika vituo vya kutolea huduma za afya. Asilimia 98 ya wajawazito huhudhuria kliniki kipindi chote cha ujauzito wao lakini ni asilimia 64 mpaka 70 pekee ndio hujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. Aslimia 24 mpaka 38 zilizobaki hujifungulia nyumbani, huku sababu kubwa ikiwa ni kukwepa manyanyaso kutoka kwa watoa huduma za afya.
Hali hii ya kuwa na kundi kubwa la wanawake wanaojifungulia nyumbani, ndiyo ambayo imepelekea nchi yetu ya Tanzania iendelee kuwa na namba kubwa ya vifo vya mama na matatizo ya uzazi ( vifo vya mama 524 kati ya vizazi hai 100,000 na vifo vya watoto 31 kati ya vizazi hai 1,000). Ikiwa hatua madhubuti hazitachukuliwa haraka, bila shaka tutaendelea kuona matatizo ya uzazi na vifo vya mama vikizidi kuongezeka.
Alisikika mama mmoja akisema “Wanawake hatuteswi na uchungu peke yake wakati wa kujifungua, maneno mabaya tunayoambiwa na yale manyanyaso tunayofanyiwa na watoa huduma, huongeza maumivu zaidi” aliongezea kwa kusema “… ni kweli wanatusaidia lakini manyanyaso wanayotufanyia, huishusha kabisa thamani ya msaada ule mkubwa wanaotupatia”. Maneno ya mama huyu, yamewakilisha maumivu makubwa yaliyobebwa na wanawake wengi mioyoni mwao kutokana na yale wanayofanyiwa wakati wa kujifungua.
Wanawake wengi hutamkiwa maneno ya aibu, wengine hupigwa vibao na inafika kipindi baadhi ya watoa huduma kuwasusa kinamama wanaojifungua kwa madai kwamba ni wasumbufu na hawaonyeshi ushirikiano. Ni mambo ambayo yanahuzunisha sana, kushangaza na kufikirisha mno. Kwa dunia hii tuliyonayo sasa, ni mambo ambayo hayakutarajiwa kama yangekuwa bado yanatokea. Hii ni aibu kubwa kwa taifa letu!
Katika kulifuatilia swala hii, nimefanikiwa kuongea na watoa huduma za afya kadhaa wakiwemo wauguzi, wakunga na madaktari. Idadi kubwa ya wataalam niliozungumza nao, walikiri kwamba ni kweli vitendo hivyo hufanyika japo havifanywi na wote. Muuguzi mmoja ambaye pia ni mkunga, aliniambia “Kuna muda huwezi kukwepa kuwa mkali, maana ukilegea kidogo unaweza ukampoteza mtoto. Kwahiyo ni bora uonekane umemdharirisha mama kwa kumnasa kibao lakini mtoto apone. Bahati nzuri, huwa wanaelewa kama tunafanya yote hayo kwa ajili ya kuwasaidia, ndio maana hata baada ya hayo tunaongea nao vizuri tu na hata tukikutana mtaani tunacheka pamoja kama kawaida”
Binafsi siamini kama kuna mtaalam yeyote wa afya ambaye amefundishwa na wakufunzi wake mbinu za kuyaokoa maisha ya mama na mtoto kwa njia ya kumdhalilisha mama. Hili ni swala ambalo halikubaliki hata kidogo na ni kinyume na taaluma yoyote ile inayohusisha masuala ya afya. Ni mhimu sana utu na heshima vizingatiwe wakati wote bila kujali ni nani na kuna nini.
Kwanini malalamiko kama haya tusiyasikie kwenye nchi zilizoendelea? Je! kule hawapitii mchakato sawa na hawa wanawake wa kitanzania wakati wa kujifungua? Kuna kitu hakiko sawa katika maeneo ya kutolea huduma za afya, kuna mstari kama nchi inayojali utu tunapaswa tuuvuke. Inawezekana kabisa watoa huduma wanaofanya mambo kama haya ni wachache, lakini uchache huo umezalisha madhara hasi ambayo ni mengi zaidi. Matokeo yake ni imani ya watu juu ya watoa huduma kuendelea kupotea.
Kila mgonjwa anapaswa kupata huduma salama, zenye ubora na staha. Tofauti na hapo ni kwenda kinyume na misingi ya taaluma yoyote ile ya masuala ya afya. Ni mhimu sana kukumbuka kuwa, kujifungua ni wajibu wa mama, lakini lolote baya analotendewa mama kipindi cha kujifungua laweza kuathiri afya ya mtoto kimwili na kiakili. Pia, afya ya akili ya mama huwa katika hatari zaidi pale anapotendewa mambo ambayo si ya kulinda utu wake hasa katika kipindi cha ujauzito, wakati wa kujifungua na baada ya ujauzito.
Nampongeza sana msajili-Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha taaluma na wanatauluma ya Uuguzi na Ukunga nchini wanasimamiwa kikamilifu. Hata hivyo, bado kunahitajika nguvu kubwa zaidi kwakuwa, pamoja na adhabu zote kali zinazotolewa kwa wale wanaokwenda kinyume na misingi ya taaluma ya uuguzi na ukunga , tunaendelea kushuhudia mambo mabaya yakiendelea kutekelezwa na wataalam hao.
Pamoja na kwamba serikali inaendelea kuboresha huduma za afya, lakini bado ipo haja kubwa ya kufanya uchunguzi wa mara kwa mara katika maeneo ya kazi ili kubaini wale watovu wa nidhamu. Ikumbukwe kwamba; hata kama huduma zikiboreshwa kwa kiwango cha juu zaidi, ikiwa watoa huduma watakosa namna nzuri ya kuwafikishia wananchi huduma hizo kwa ubora unaotakiwa, basi juhudi zote za serikali na wadau husika zitakuwa hazina maana yoyote.
Binafsi nafikiri tumeufikia wakati sahihi ambao wanaume wanapaswa wawe huru kuingia moja kwa moja kwenye chumba cha kujifungua wakati wake zao wakiwa huko. Hii itasaidia sana kupunguza hatari ya wake zao kunyanyaswa wakiwa katika hatua ya kujifungua. Lakini pia, ni vyema jamii ielimishwe juu ya ubora wa huduma wanazopaswa kupewa na wapi wapeleke malalamiko yao pale wanapokuwa hawajaridhishwa na aina ya huduma walizopewa.
Kama ningefanikiwa kukutana na watoa huduma wote wa afya ningewaambia yale maneno ya Lewis Carol yanayosema “Moja ya siri kubwa sana katika maisha ni kwamba, mambo yote ambayo ni mhimu sana kwetu kufanya ni yale matendo bora tunayowafanyia wengine”
Ahsanteni sana!

Upvote
1