Unyanyasaji, ukatili anaofanyiwa Mtoto unaweza kumfanya awe mkatili

Unyanyasaji, ukatili anaofanyiwa Mtoto unaweza kumfanya awe mkatili

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
100_7036.jpg
Kutokana na matukio mfululizo wa mengi ya unyanyasaji wa kijinsia hasa ubakaji na ulawiti kuendelea kuripotiwa, Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Aifello Sichalwe anafafanua matukio hayo kitabibu yanaathiri vipi jamii na wale wanaotendewa uhaifu huo:

Kunakuwa na uhatarishi wa maambikizi ya Magonjwa mbalimbali kama vile VVU (HIV), Hepatitis, Kaswende n.k

Kuna ambao wanakuwa wameanza kupevuka na wanaweza hata kupata ujauzito katika umri mdogo.

Majeraha katika maeneo ya siri kutokana na udogo wao, lakini pia wanaweza kupata majeraha kutokana na nguvu inayotumika kumdhibiti.

Wapo ambao huwa wanauawa ili kuziba asiweze kusimulia ukatili uliotendeka.

Kwa wale ambao wanafanyiwa ukatili wa kimwili huwa wanaweza kupoteza viungo kutokana na ukatili wanaokutana nao...

Upande wa kisaikolojia anasema mwathirika wa ubakaji anaweza kupata changamoto mbalimbali za Afya ya Akili kuanzia msongo wa mawazo, PTSD, personality disorders, ulevi uliopitiliza na pia yeye mwenyewe kuwa mkatili.
 
Back
Top Bottom