Habari za muda huu ndugu zangu.
Kwa kweli Kwa Hali ilivyo, inabidi jambo kubwa sana lifanyike katika nchi yetu kubadili mifumo yetu ya ulinzi na usalama wa raia.
Asubuhi ya Leo, nasikiliza Power Breakfast ya Clouds FM, kuna habari ya kijana ISSA, ambaye amefanyiwa ukatili uliopitiliza na kuondolewa utu wake. Kijana kapigwa, katobolewa kwenye koo na vitendo vingine kinyume na ubinadamu.
Sababu ni tuhuma za kijana Kuiba TV, ambapo Askari wa kituo cha Goba walitaka rushwa ya laki nane. Mama akaomba punguzo Hadi laki tano. Lakini PESA haikutumwa kwakua wazazi walitaka itumwe kwa namba ya Askari, lakini Askari wakagoma na kutaka itumwe Kwa namba ya mtuhumiwa.
Kinachoumiza zaidi ni majibu ya dharau na kejeli ya IGP Sirro na Ramadhani Kingai.
Mwandishi alipomhoji Sirro, Sirro alimjimu kama amemuona na ana udhibitisho. Mwandishi akamjibu ndio, Sirro kuona hana cha kujitetea akamwambia amtafute kamanda wa Kinondoni.
Kingai yeye anaongelea kwa wepesi tu kwamba kijana yupo hospitali na watamfungulia mashtaka.
Kwa kweli watu hawa (Polisi), Kwanza ndo wanaongoza Kwa vitendo vya kikatili na ugaidi dhidi ya watu na Mali zao. Hawana weledi katika kazi na hawazijui kanuni za kazi yao.
Huyu IGP amekuwa na Ile mentally ya awamu iliyopita, ya uongo, chuki na uonevu. Na Kingai ni mtekelezaji WA vitendo hivyo.
Hawa ndio waliomshauri Mama vibaya kuhusu Mbowe na kumpelekea kuonekana Mwongo, kinyume na dhamira yake. Wanahitajika kupumzishwa.