Imefika wakati ni bora utupwe kwenye kundi la Simba ujue moja labda watakuacha kama wameshiba, kuliko ujikute mikononi mwa hao polisi wenye njaa isiyoisha, utajuta.
Kwa tabia ukali aliyoonesha huyo Kingai pata picha uko chini yake anakulazimisha ukiri atakacho, mateso, vipigo, matusi, ni halali yako mpaka pale utapokiri umekosa hata kama kimsingi hujakosa, wale kina Adamoo ni mashahidi wazuri sana wa hiki nachoandika.
Tatizo wamelelewa na CCM kwa tabia hizo, kuwatesa wapinzani kwa manufaa yao, matokeo yake sasa polisi wame extend unyama wao mpaka kwenye matukio nje ya siasa, wanajua watalindwa na mabosi wao wa CCM, sasa nashangaa kada wa lumumba unakuja kulalamika kwa tatizo mlilolizaa na kulilea wenyewe.