Unyanyasaji wa kijinsia mtandaoni unawanyima Watu wengi kupata fursa zilizoko huko mtandaoni

Unyanyasaji wa kijinsia mtandaoni unawanyima Watu wengi kupata fursa zilizoko huko mtandaoni

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,455
Reaction score
5,134
Unyanyasaji wa kijinsia mtandaoni unawanyima Watu wengi kupata fursa zilizoko huko mtandaoni

Mtandaoni kuna fursa nyingi lakini wapo weni wanaoogopa kuwa mtandaoni kwa kuongopa unyanyasaji ambao wengine huufanya wakiamini kama sehemu yao ya burudani.

Mfano kuna dada mmoja nilipata fursa ya kuzungumza naye kuhusu fursa za kiuchumi mtandaoni, alichonijibu ni kuwa "naogopa kurudi tena mtandaoni kwani niliwahi kupost picha yangu nikitaka watu wanipongeze kwa kuwa ilikuwa siku yangu ya kuzaliwa, mwanzo walijua kwa picha za bandia ila nikaona niwe halisi, nilivyopakia picha yangu nilijuta.

Hali ilikuwa tofauti na matarajio kwani niligeuka kuwa trending ya siku kwa kuchekwa huku wanaokomenti na kushea wakisema nina sura mbaya, ya baba, nina pua kubwa nk. Picha yangu ilitengenezwa Meme na mpaka leo inatumika kudhalilishia wengine,

Natambua umuhimu wa mtandao lakini watu hutumia kama sehemu yao ya kudhalilisha wengine kwa muonekano wao au jinsia yao kwani mmoja alinifata DM akanambia Mwanamke unakuwaje mbaya hivyo? Kama hukutaka kuwa mwanamke si ungesema tu"

Kwa hali kama hii, ni watu wangapi wanaogopa kutumia itandao kisa ukatili wa kijinsia mtandaoni?

Wakuu tuachane na kudhalilisha watu mitandaoni ili wote kama jamii tutumie fursa zilizoko huku.
 
Kama ulivyosema mtandaoni ukitumia kwa biashara inalipa sana kuliko maisha binafsi, huyo uliyemuonyeshea mfano angesifiwa usingesikia hayo aliyosema, ukishaanza kuweka personal information mtandao ni mbaya kuliko
 
Back
Top Bottom