ElizaMwaki
Member
- Sep 23, 2021
- 6
- 6
Unyanyasaji wa wenza majumbani ni aina ya Unyanyasaji wa Kijinsia unaohatarisha afya ya umma ulimwenguni kote na huletelea madhara kisaikolojia, kiuchumi na kiafya kwa mtu binafsi, familia na jamii.
Unyanyasaji wa wenza majumbani ni tabia ya ndani ya mahusiano ya kimapenzi zinazoletelea madhara kimwili, kingono au kisaikolojia na mpenzi wa sasa au wa zamani. Inajumuisha kulazimishwa kingono, unyanyasaji wa kisaikolojia na tabia ya kumdhibiti mwenza.
Asilimia thelathini (30%) ya wanawake duniani ni waathirika wa unyanyasaji wa wenza. Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha asilimia thelathini na nane (38%) ya wanawake nchini Tanzania wanakabiliwa na ukatili (Shirika la Afya Duniani, WHO)
Ingawa hakuna ripoti nyingi za unyanyasaji wa wanaume unaofanywa na wanawake, kuwepo kwake hakuwezi kukanushwa. Asilimia saba (7%) ya wanawake kutoka maeneo ya mjini, Tanzania, wameripotiwa kuwakatili wenza wao. Hata hivyo, kwa tamaduni zetu si rahisi mwanamke kukubali kumkatili mwenza wake wala mwanaume kutoa taarifa iwapo amekatiliwa, idadi ndogo ya kesi za wanaume kunyanyaswa na wanawake zinaletwa na kutoripotiwa kwa matukio ya ukatili dhidi ya wanaume.
Pamoja na hayo, bado kuna idadi kubwa ya kesi za ukatili dhidi ya wanawake inayotatiza. Kwa mujibu wa habari kutoka gazeti la ‘THE CITIZEN’, wadau wa haki za binadamu wametaka hatua za kuthibiti ukatili dhidi ya wanawake ziongezwe kutokana na ongezeko la kesi kati ya mwaka 2017 hadi 2019. Unyanyasaji wa majumbani na utumiaji wa lugha za kejeli, kubeza na matusi umebainika kuwa tatizo kubwa zaidi.
Sababu zipi hatarishi hupelekea Unyanyasaji wa wenza majumbani?
Sababu hatarishi zinazoweza pelekea kuwepo na unyanyasaji wa wenza zimegawanya katika makundi matatu;

- Sababu za mtu binafsi ni zile hulka, tabia na historia ya mtu inayoongeza uwezekano wa kuwa muathirika au katili. Umri mdogo, kiwango duni `cha elimu, mitazamo au imani zinazounga mkono aina yoyote ya unyanyasaji, historia ya kunyanyaswa au kushuhudia unyanyasaji utotoni, matumizi mabaya ya pombe na/au dawa za kulevya.
- Sababu zitokanazo na mahusianoya mtu kupitia marafiki, familia au mpenzi yenye migogoro ya ndoa au kutoridhika ndani ya mahusiano, ndoa za kupangwa au kulazimishwa, wapenzi wengi, dhiki ya kiuchumi, tofauti kubwa ya kiwango cha elimu kati ya wenza, kuwa na marafiki katili na kuwa katika familia yenye mazingira ya mfumo dume kali.
- Sababu za kijamii ni zile zinazohusisha mahusiano ndani ya taasisi za elimu, mahali pa kazi na ujirani. Hizi ni pamoja na umaskini, ukosefu wa msaada kutoka kwa polisi au mfumo wa mahakama, njia dhaifu za kuthibiti wahalifu na uvumilivu wa matendo ya unyanyasaji wa kijinsia. Uwepo wa mila na desturi zinazoruhusu unyanyasaji na/au ukosefu wa usawa kwa mfano wanaume kuchukuliwa ni jinsia bora kuliko wanawake.
Unyanyasaji wa wenza majumbani hutokezea madhara yapi?
- Majeraha kama michubuko, vidonda, kuvunjika mifupa, majeraha ya ndani ya tumbo na kifua, majeraha ya kichwa ambayo huleta uharibufu wa macho, masikio na ubongo. Magonjwa ya baadae kama maumivu ya mwili ya muda mrefu.
- Kuzorota kwa afya ya akili, ustawi na kujiua. Uchunguzi umeonyesha kuwa waathiriwa wa unyanyasaji wanakabiliwa na sononi, woga, mihemko na mawazo ya kujiua. Unyanyasaji wa wenza majumbani pia hupelekea matumizi mabaya ya vileo na kutojithamini.
- Madhara ya afya ya ngono na uzazi ni pamoja na mimba zisizotarajiwa, utoaji na kuharibika kwa mimba, magonjwa ya zinaa yatokanayo na kulazimishwa kujamiiana na kuzuiwa kutumia njia za kuzuia maambukizi.
- Kuongezeka kwa vifo. Waathiriwa huishia kujiua au kuuwawa baada ya kukatiliwa kwa kipindi kirefu. Pia waathiriwa huamua kukatiza maisha ya wanaowakatili au kuwajeruhi vibaya sana.
- Kuzorota kwa maendeleo ya jamii kutokanako na afya duni inayokwamisha na kupunguza uzalishaji na kipato. Waathiriwa wanashindwa kujihusisha na majukumu yao ya kila siku kwa ufanisi.
Madhara gani huwapata watoto?
Wakati mafarakano yanapotokea baina ya wazazi/wenza, watoto huangukia kwenye mzozo. Hii hupelekea watoto kuathirika kimwili na kisaikolojia. Athari ni kama;
Wakati mafarakano yanapotokea baina ya wazazi/wenza, watoto huangukia kwenye mzozo. Hii hupelekea watoto kuathirika kimwili na kisaikolojia. Athari ni kama;
- Hali ya woga na bumbuazi
- Hali ya sononi
- Ugonjwa wa mkazo baada ya kiwewe
- Kuhisi kuachwa na kutopendwa
- Utoro na ufaulu duni shuleni
Watoto ambao wazazi wao hutengana/kutalikiana au kufariki;
- Hukabiliwa na migogoro ya kujitambua
- Hukosa mapenzi ya mzazi mmoja
- Wengine huishia kwenye vituo vya malezi, mitaani na kuwa wahalifu.
Je, tunakilindaje kizazi kijacho?
Kutokomeza unyanyasaji wa majumbani ni muhimu ikiwa tunataka watoto wetu wakue katika mazingira ya afya njema. Ingawa juhudi nyingi zimetumika kwa miaka mingi, kuna haja ya kuziongeza;
Kutokomeza unyanyasaji wa majumbani ni muhimu ikiwa tunataka watoto wetu wakue katika mazingira ya afya njema. Ingawa juhudi nyingi zimetumika kwa miaka mingi, kuna haja ya kuziongeza;
- Kubuni programu mashuleni kuwafunza watoto juu ya aina za unyanyasaji wa kijinsia, madhara yake na jitihada za kutokomeza. Kujumuisha tarehe ya siku ya usawa wa kijinsia katika kalenda za shule. Siku hii iwe ya kujifunza na kupata stadi za maisha.
- Kuundwa kwa vikundi vya majadiliano juu ya usawa wa kijinsia ili kuzalisha mitazamo chanya inayokuza usawa wa kijinsia na kutokomeza mila kandamizi zinazochochea ukatili.
- Kuhamasisha jamii kubadili tabia na fikra zinazopelekea na kuchochea unyanyasaji kwa njia ya mzungumzo kupitia ziara za nyumba kwa nyumba, vikundi, vyombo vya habari na viongozi wa dini.
- Kubuni mashindano ya sanaa na michezo mfano mbio, ligi za kandanda, uandishi wa insha, uigizaji na nyimbo yatakayoshirikisha vijana wa kike na wa kiume ili kuongeza uelewa na jitihada za kuzuia unyanyasaji.
- Kuhakikisha uwepo wa mfumo thabiti wa kuhudumia waathiriwa na watoto wao kwa kuweka sera na miundombinu inayolinda faragha na usiri wa mwathiriwa.
- Kuhamasisha na kutoa mafunzo kwa Jeshi la Polisi juu ya kuboresha Dawati la Jinsia katika kushughulikia kesi na tuhuma za unyanyasaji wa wenza majumbani.
Afya na ulinzi wa watoto ni wajibu wetu. Tutengeneze mazingira yatakayowezesha watoto wetu wakue vema na kujenga maisha kwa amani. Watoto wetu wakistawi, taifa letu litastawi.
Upvote
10