Deogratias Mutungi
Senior Member
- Oct 1, 2019
- 141
- 183
Salaam wana JF.
Nianze andiko hili kwa kusema kuwa ushindi wa kishindo wa Chama Cha Mapinduzi CCM katika uchaguzi wa mwaka huu utatokana na nguzo imara za "Unyenyekevu, Utu, Uwajibikaji, Uchumi, haki na Amani ya Nchi, hizi ndizo hoja za msingi wa kuipa kura CCM Bara na Visiwani wala si vinginevyo"
CCM kupitia falsafa zake wameweza kufanikisha hili kwa weledi wa hali ya juu katika utumishi wa wananchi ndani ya taifa hili. Hoja hii haina itikadi wala ukada wa chama chochote bali uzalendo wa taifa letu. Wanaharakati na Wapinzani wa vyama vya siasa wanalitambua hili kulingana na kazi za serikali ya CCM toka awamu ya kwanza hadi sasa awamu ya tano
Waswahili wanasema myonge myongeni lakini haki yake mpeni. Kwa kazi iliyofanywa na Chama Cha Mapinduzi kwa awamu zote hasahasa awamu hii ya tano Watanzania tunao wajibu wa kumpa kura za ndio kwa wingi Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ili aendelee kuwatumikia Watanzania kwa weledi na ubunifu wake wa miradi ya maendeleo kama alivyo fanya ndani ya miaka mitano.
Aidha, Taifa lolote lile duniani linahitaji nguzo imara za Unyenyekevu, Utu, Uwajibikaji, Uchumi, Amani na haki ili liweze kustawi na kujiendesha lenyewe wala hii sio propaganda bali ni ukweli ulio wazi kuwa Tanzania kupitia Chama dola CCM na falsafa zake za kijamaa wameweza kufanikisha maendeleo ya watu kwa hatua kubwa zinazogusa kila unyayo wa Mtanzania wa taifa hili
Tuna Chama imara kinachojipambanua katika sera, mifumo na mikakati inayokubalika katika kutatua kero za watu wake, ndani ya karne hii na siasa za Kiafrika uwezi kuilinganisha CCM na Chama chotechote kile katika utumishi wa umma na falsafa zake za maendeleo.
Kwa mantiki hiyo Watanzania tunao wajibu wa kuirudisha madarakani serikali ya Chama Cha Mapinduzi hili amani, haki, uchumi na maendeleo ya watu na vitu yaendelee kutamalaki ndani ya taifa letu na jamii zetu kwa ujumla, tunao wajibu wa kuchagua viongozi wenye kuguswa na matatizo ya watu wake na wenye uwezo wa kuyasikia na kuyatatua kwa wakati,
Chama Cha Mapinduzi CCM wanao uwezo na nia ya kufanya hivyo, kwa lugha hiyo tumtume tena Dkt. John Pombe Magufuli kwa upande wa bara na tumpe kura za ndio kwa wingi Dkt. Hussein Mwinyi kwa upande wa Zanzibar
Ni rai ya andiko hili kuwa Watanzania wataiamini CCM na kuipa ridhaa ya kuwatumikia tena kwa miaka mitano.