Unyonyaji unaofanywa na Diamond/WCB kwa wasanii hauna tofauti na ule wa Clouds na waliekuwa wanamtuhumu

Unyonyaji unaofanywa na Diamond/WCB kwa wasanii hauna tofauti na ule wa Clouds na waliekuwa wanamtuhumu

mwanamabadiliko

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2010
Posts
938
Reaction score
1,540
Uongozi wa WCB chini ya Diamond ni moja kati ya lebo inayowanyanyasa na kuwanyonya wasanii wake na kuwasainisha mikataba ya kina Chief Mangungo isiyokuwa na haki na iliyojaa unyonyaji wa kupita kiasi.

Ni hawa hawa waliokuwa wanailalamikia clouds kupitia na wakurugenzi wao kuwa ni wanyonyaji, lakini wanachofanya wao bora hata Clouds.

Msanii Rich Mavoko ameondoka coz ya kunyonywa, Hamonaizi ameondoka na mdeni wa mil 500 mpaka kupelekea nyumba zake kupigwa mnada. Rayvanny na Lavalava wanalalamika chini chini, na huenda huu mwaka usiishe watakuwa washajitoa.

Diamond si mtu mzuri, alimnyanyasa sana Mwarabu Fighter,. Pia ni lazma awanyonye kama baba yake tu aliemtoa kiunoni kwake alimnyanyasa ndo ije Rayvanny na Mavoko.

Tubadilike jamani WCB
 
Kama hujui terms za mikataba ya wasanii, ni bora ungekaa kimya tu usubiri wenye uelewa kuhusu hili waanzishe nyuzi... Kum-manage msanii sio kazi ndogo kama wengi wanavyofikiri, hasa ikiwa msanii bado mchanga kabisa. Hii migogoro ya mikataba kati ya msanii na management yake iko duniani kote...

Ndio maana pale WCB mtu yeyote anayetoka pale au hata fununu tu kuwa anataka kuachana na lebel, huwezi kukuta Diamond anaongelea popote, hajawahi kuzungumza lolote kuhusu Kifesi, Mwarabu fighter, Q boy, Rich Mavoko na hata huyu Harmonize wa juzi Diamond hatazungumza chochote... hujiulizi kwa nini anakaa kimya pamoja na watu wengi kutamani aseme neno?
 
Usilolijua ni sawa na usiku wa Giza ,nadhani hao unaosema wananyonywa wakati wanasign mkataba walikua na akili timamu na walisoma kwanza wakaelewa kila nukta na mda pia wa kufikiria walipewa
 
Diamond huyu huyu unayesema mnyonyaji alimchukua harmonize wa Maraika akampika kwa miaka miwili pale usafini akamjengea heshima na kumtetea akahakikisha kijana anatoboa kimataifa akamkingia kifua Mawingu wasimtumie bure kwa kupandisha thamani yake.

Kumbuka alipochukuliwa hakua na uwezo wa kununua hata wa 1m lakini kupitia Diamond Harmonize amekua star,pesa,timu kubwa na uwezo wa kuwanunulia mpaka wazazi wake magari je,ulitaka diamond afanye nini zaidi ya hapo au ulitaka awe ana mpa na hela zake za shoo?

Clouds wasanii wao wote hakuna hata msanii mmoja waliowahi kumfanyia hayo yote zaidi ya kuwatumia na kuwaacha.Hata kama Diamond mnyonyaji kama unavyosema basi mara kumi yake yeye kuliko hao mawingu.
 
Uongozi wa wcb chini ya diamond ni moja kati ya lebo inayowanyanyasa na kuwanyonya wasanii wake na kuwasainisha mikataba ya kina chief mangungo isiyokuwa na haki na iliyojaa unyonyaji wa kupita kiasi.
Ni hawa hawa waliokuwa wanailalamikia clouds kupitia na wakurugenzi wao kuwa ni wanyonyaji, lakini wanachofanya wao bora hata clouds.
Msanii rich mavoko ameondoka coz ya kunyonywa, hamonaizi ameondoka na mdeni wa mil 500 mpaka kupelekea nyumba zake kupigwa mnada. Rayvanny na lava lava wanalalamika chini chini, na huenda huu mwaka usiishe watakuwa washajitoa.
Diamond c mtu mzuri, alimnyanyasa sana mwarabu fighter,. Pia ni lazma awanyonye kama baba yake tu aliemtoa kiunoni kwake alimnyanyasa ndo ije rayvany na mavoko.

Tubadilike jamani wcb
98% hawatasapoti ulichoandika maana umeandika ushundu na imeonesha kiwango chako Cha elimu kipo chini umeaibisha jukwaa la great thinker naona somo la LAW OF CONTRACT limekupitia pembeni.
 
Back
Top Bottom