BAK...siamini hata kidogo eti binti amejitunza vizuri na anampenda Mungu, akose mume wa kumuoa...:A S 13:. Wapo wanaume pia wanaopenda mabinti waliotulia, ambao hawaonjeshi kwa kila mtu, kwa hiyo atapata tu!
Tatizo ni upungufu wa imani, ukimuomba Mungu kwa moyo safi basi nae atakupatia Mume bora au mke bora. Ila tatizo watu imani zao zimekua haba.. Watu tunatumia akili zetu kuliko kumtegemea Mungu.. Na hili ndo tatizo kubwa, ila nadhan na mmomonyoko wa maadili nao umechangia, nadhani babu zetu walikuwa wanachakachuana baada ya kuoana.
Acha kuwachuuza wenzio, kuna mfano live mtaani kwetu, binti mmoja mtaani, kila vijana wakijitokeza kutaka kuja kujitambulisha wanakimbia kimyakimya... kuja kugundua tatizo hataki wa confirm kama kweli bidhaa inalipa... sasa hivi anatafuta 40 wadogo zake wote wa kike wameolewa!!! Mtu utauziwaje mbuzi kwenye gunia, ukishaoa ukaenda usiikute inapotakiwa iwe!!!! :A S 13::A S 13:
Dunia imetaharuki!!!
Kwa ulimwengu huu ulivyo ni afadhali mara mia mbili, ukajua unaingia na nani humo ndani,
hata umfahamu kwa sehemu tu.
Hapana, dunia ya kuenenda kwa Imani naona inafikia mwisho.
Sijui ndo mwisho wenyewe huu, mmmh utamaso na ulaghai umejaa sana.
Watu wote wanaotetea imani hapa kama wamewahi kua na mahusiano ya kimwili na mwanaume/mwanamke then ni unafiki!!!Huwezi kupinga watu wawili kuishi pamoja eti kwasababu hawajaona wakati wewe una mahusiano ya kimwili na mtu wakati hamjaoana!!!
Tofautisheni ndoa na fomalities za ndoa, hata kama mna timu ya futbolli kama hamjaweka nadhiri ya kuishi pamoja nyinyi hmjafunga ndoa, na hata kama hamjachakachuana au shake well before use haijapita mkafungishwa ndoa lakini kila mmja anamlengo yange mbele za Mungu hiyo si ndoa , Mungu anaibariki ndoa iliyohalali ikiwa mioyo ya wawili hao imekubaliana kabisa, so kama wamechakachuana au la iyo shauri yako, kama huwezi kuchakachua subiri muda wako ukifika upate mwenza, lakini atakuwa kachakachuliwa na wenzio................. kagabaho na............................
Ndo uonje mara kumi?Tatizo ni kwamba walioweng wana2mia njia hiyo kuwaharibu wasichana hawana nia
mh,so kama ulikosea then ukaijua njia sahihi na unawashauri wasifanye hivyo huo nao unafiki?na kuna kutofautiana opinion my dear,si unafiki...and by the way mtu halazimishwi kuchukua kila analoambiwa,at the end ni uamuzi wa mtu binafsi......anyway,sikujua kusema kitu tofauti na wengine hata kama uliwahi kuwa hivyo ni unafiki....am out!
kumfahamu mtu haiminishi uishi naye kwanza. Nafikiri kipindi cha uchumba hadi ndoa, bado mnaweza kusomana tabia. Kuambiana ukweli ni kitu muhimu, na pia kuwaona madaktari ili kuona kwamba mtahili vishindo mkiwa chumbani.
Hakuna sababu ya kuhalalisha kuishi maisha ya unyumba kabla ya ndoa. ni upungufu wa imani.
Ni muhimu kumjua mtu kabla hamjaoana!Ndo maana watu wanaobebana tu baadae kila mmoja anaanza sikujua yuko hivi..ningejua kumbe yuko vile!Kidini sio sawa ila katika ulimwengu wa leo ni muhimu sana!
YaPO MAMBO YA KUTESTI KAMA CHUMVI KATIKA MBOGA,CHAI KAMA SUKARI IMEZIDI AU LAA! ILA CO UCHI, HAYA MAMBO MAZITO JAMANI,KATIKA DHAMBI KUBWA NI II, MANA AMELAANIWA YULE ATENDAYE DHAMBI JUU YA MWILI WAKE MWENYEWE(KUZINI) SASA MNAOSEMA LAZMA KUPMA KAMA PANA LIPA AU LAA CJUI NI WA DINI GANI TUJISAHIHISHE WAJUMBE!
Hebu soma mstari huu hapa Mpendwa:
Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo,
kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu. Efeso 3:20.
Tukumbuke kwanza tunaokolewa kwa neema, na Imani juu ya Mungu huja kwa kusikia na kusikia huja kwa neno la Mungu.
Tukumbuke kiwango cha Imani na nguvu ya Imani ndani ya mtu inatofautiana. Na Mungu anafanya mambo kadiri ya nguvu iliyopo ndani yako.
Ninachotaka kusema ni nini? Tusiwe na haki kupita kiasi, Kila mtu hapa duniani ana njia yake ya kupita, kuna mtu mmoja anaitwa Hosea aliambiwa aende akaoe mzinzi fulani hivi. Fuatilia ukoo wa Yesu, usome habari za Ruthu, Rahabu, na wengine.
Sasa basi kwa kuwa dunia imezungukwa na mambo mengi, siweze kumlazimisha mtu aamini kama ninavyoamini mimi, hasa kwenye swala la mahusiano, hili swala limekaa kimwili zaidi, mnisamehe!! Hakuna kuhubiri injili humo ndani, wala kuimba mapambio. Sasa ukikutana na huyo asiyeweza sijui utaishi naye kwa Imani, wakati kama ungemfahamu mapema ungefanya uamuzi mapema??
Huko ni kujidanganya tena sana. Wewe unadhani tabia ya mwanamke au mwanaume kabla ya kuoana itakuwa sawa na baada ya kuoana rasmi? Kalagha bakho!! Kwani kujuana maana yake ni kulala pamoja!! Kama ni shetani basi amekutawala kwelikweli.
huo ndio mpango mzima dena.
Tena hadi mimba ishike ndio tutangaziane ndoa.
hakuna mwenye haki hata mmoja. hata Biblia hiyo hiyo inasema 'wote wamepungukiwa na utukufu wa Mungu'.. tunaokolewa kwa neema. Wala sitaki kumaanisha kwamba mawazo yangu ndio kila kitu. hapana. Ninaoandika ninayoyaamini.
Nafikiri kama umeweza kukubali kuishi na mtu kwenye nyumba moja, sioni point ya kutest hapo.
Kuna namna nyingi tu za kumjua mtu kulingana na unavyoona wewe. Sifikirii kwamba ni lazima uishi naye kwanza. that was my point.
sote hapa tunajifunza, ni mtu mwenyewe anaamua achukue kipi na aache kipi. These are my opinions.
Huko ni kujidanganya tena sana. Wewe unadhani tabia ya mwanamke au mwanaume kabla ya kuoana itakuwa sawa na baada ya kuoana rasmi? Kalagha bakho!! Kwani kujuana maana yake ni kulala pamoja!! Kama ni shetani basi amekutawala kwelikweli.