Hebu soma mstari huu hapa Mpendwa:
Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo,
kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu. Efeso 3:20.
Tukumbuke kwanza tunaokolewa kwa neema, na Imani juu ya Mungu huja kwa kusikia na kusikia huja kwa neno la Mungu.
Tukumbuke kiwango cha Imani na nguvu ya Imani ndani ya mtu inatofautiana. Na Mungu anafanya mambo kadiri ya nguvu iliyopo ndani yako.
Ninachotaka kusema ni nini? Tusiwe na haki kupita kiasi, Kila mtu hapa duniani ana njia yake ya kupita, kuna mtu mmoja anaitwa Hosea aliambiwa aende akaoe mzinzi fulani hivi. Fuatilia ukoo wa Yesu, usome habari za Ruthu, Rahabu, na wengine.
Sasa basi kwa kuwa dunia imezungukwa na mambo mengi, siweze kumlazimisha mtu aamini kama ninavyoamini mimi, hasa kwenye swala la mahusiano, hili swala limekaa kimwili zaidi, mnisamehe!! Hakuna kuhubiri injili humo ndani, wala kuimba mapambio. Sasa ukikutana na huyo asiyeweza sijui utaishi naye kwa Imani, wakati kama ungemfahamu mapema ungefanya uamuzi mapema??