Hii karata ya 'kupora mke wa mtu' CCM wamejaribu kuicheza kwa kutumia magazeti ya kipuuzi kama Mtanzania na Rai, lakini wapi! Naona kweli watanzania sasa wameamka. Tunataka Rais mwenye uthubutu wa kuzuia uporaji wa raslimali zetu, basi. Sisi hatujali kama ana hawara au anatembea na mke wa mtu. Tumegundua kwamba huyu anayetaka tena miaka mingine mitano hana uwezo wa kuzuia uporaji wa raslimali zetu kwani waporaji ni marafiki zake wakubwa. Sasa anataka tumchague ili....?? NGUVU YA UMMA ndio silaha yetu pekee katika kuondokana na unyonyaji huu unaotufanya tuwe maskini katika nchi tajiri.