Unywaji wa mafuta gari ndogo

Unywaji wa mafuta gari ndogo

Mwenyewe nilitegemea hivyo na hii vitz new model, ila imenisikitisha sana kutembea 9.7km/L , hili ni tatizo ambalo bado sijafahamu solution
Hapo mkuu, kama upo serious kuna uwezekano wa kucheki gari kwa fundi.

Average yako ilitakiwa iwe 14-16 hapa town, ukienda mkoa iwe juu ye 20+
 
Ulaji wa mafuta wa gari unategemea Vitu vingi hata iwe gari ndogo Kama ist

1.Ubora wa barabara , unatumia njia gani Mara kwa Mara Mana matumizi ya kuendesha lami na off-road Ni tofauti.

2. Ubora wa matairi, kuweka tairi au rims tofauti na maelekezo ya mtengenezaji , sometimes inachangia.

3. Kuweka mafuta ya kuunga unga, Lita 2 Mara Lita 3 Mara moja , kwa ufahamu wangu gari ikiwa na mafuta mengi inatumia vzr kuliko yenye mafuta kidogo.

4. Aina ya uendeshaji , jaribu kuendesha usizidi rpm 2,000 Yani gari ijiongeze speed yenyewe hii inasaidia

Hayo yote Ni nyongeza tu au kukumbusha ilihali najua wengi mnaendesha vizuri na kuzingatia service

Tofauti ya gari ndogo zinazotumia 1NZ engine consumption ya 12km per liter Ni constantly Japo engine ikiwa Bado mpya kabisa na yenye matunzo yote ndo inaweza kufika hizo 18km.
 
Back
Top Bottom