Mdau wa JamiiForums amedai kuwa jamii za wafugaji ni warefu kwasababu wanakunywa sana maziwa tofauti na jamii za watu wasiotumia maziwa.
Amebainisha baadhi ya sababu ni kutokana na maziwa kuwa na madini ya calcium na vitamini D ambavyo husaidia kutengeza na kuimarisha mifupa. Kinyume chake kwa jamii za wakulima ambazo hazitumii sana maziwa huwa wanakuwa wafupi.
Jambo hili lina ukweli kiasi gani?
Amebainisha baadhi ya sababu ni kutokana na maziwa kuwa na madini ya calcium na vitamini D ambavyo husaidia kutengeza na kuimarisha mifupa. Kinyume chake kwa jamii za wakulima ambazo hazitumii sana maziwa huwa wanakuwa wafupi.
Jambo hili lina ukweli kiasi gani?
- Tunachokijua
- Maziwa yana kazi nyingi mwilini ikiwemo, kujenga na kulainisha ngozi, kuimarisha meno, kuimarisha mifupa na kujenga misuli. Pia, huwa na kiasi kingi cha protini, virutubisho vinavyotumiwa kama kiini cha utengenezwaji wa vichocheo (Homoni) na kingamwili, kuponya majeraha pamoja na kutoa nishati wakati.
Maziwa yanaongeza urefu wa kimo?
JamiiForums inatambua kuwa urefu wa mtu huchangiwa kwa sehemu kubwa na vinasaba vya kurithi kutoka kwa wazazi au ukoo wake. Kwa mujibu wa maelezo ya kitaalam, chembe za urithi huchangia kiasi cha hadi 80% ya urefu wa binadamu.
Aidha, maziwa yamebeba kiasi kikubwa cha madini ya calcium, magnesium na Phosphorous ambayo hutoa mchango mkubwa kwenye utengenezwaji wa mifupa imara. Ni chakula muhimu kwenye kujenga mifupa thabiti iliyo na nguvu, isiyo vunjika kirahisi.
JamiiForums inafahamu kuwa maziwa huwa na uwezo wa kuchochez uzalishwaji wa IGF-1, homoni inayofanana na insulin ambayo pamoja na kazi zingine huuwezesha mwili kujenga misuli imara na kuongeza ukuaji.
Pia, kwa mujibu wa tafiti, unywaji wa maziwa mengi unaweza kusababisha ongezeko la urefu wa kimo kwa binadamu.
Kwa kurejea maelezo mbalimbali ya kitaalam, JamiiForums inachukulia jambo hili kama nadharia inayopaswa kuchunguzwa zaidi kwani pamoja na uwepo wa uthibitisho kuwa kimo cha mtu huchangiwa na taarifa za urithi kwa zaidi ya 80%, zipo pia tafiti chache zinazobainisha mchango wa lishe, ikiwemo matumizi ya maziwa katika kuongeza kimo.