DOKEZO Uonevu uliokithiri Idara ya Elimu Manispaa ya Moshi

DOKEZO Uonevu uliokithiri Idara ya Elimu Manispaa ya Moshi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Wewe ni mpumbavu sana tena kada wa CCM kabisaa.......mods naomba nisipigwe BAN nimepitiwa
Kwa taarifa yako tangu mwaka 1994 mimi siko ccm siwezi kuwa kwenye unafiki mimi ila naheshimu utu wa mtu wewe unatakiwa umjuwe kwanza Mungu jambo hutaki utendewe usimtendee mwenzio mimi nimekuwa chadema tangu kichanga ningekuwa mpenda madaraka ningekuwa nafasi za mwanzoni lakini mimi nimeitangaza sehemi za ndani vijini huko
 
Mimi ni Mwl. Kutoka Manspaa ya Moshi ambaye ni muhanga wa matukio machafu yanaofanywa na Kiongozi wa idara ya Elimu Ndugu NICHOLAUS NGONYANI.

Nimeandika ujumbe huu kwa uchungu na masikitiko makubwa kwa kuona kada yangu ya Elimu inachafuliwa kwa uzembe na tamaa za uongozi.

Yafuatayo ni baadhi ya Maudhi ambayo yamefanyika katika Halmashauri ya MANISPAA YA MOSHI katika Idara ya Elimu.
  • Kuomba pesa kwa Walimu Wakuu na Maafisa Elimu Kata kiwango cha kuanzia Tsh 100,000 hadi 200,000/=
  • Kutembea Na Baadhi Ya Walimu /Wake Za Watu Mfano shule za Uhuru,Kiboriloni,Mjipya,Kibo na Karanga
  • Kutoa nafasi za uongozi – Uratibu /ukuu kwa kupokea rushwa ya ngono na fedha, fuatilieni mkuu wa Kibo S/Msingi.
  • Kupeleka miradi kwenye shule za marafiki zake tu ili apate 10% ya fedha za mradi ( kwa kurudiarudia mfano Shirimatunda /Uhuru /Mgereza/Pasua /Njoro)
  • Kutishia, kufadhaisha na kuwatesa walimu kwa kuwafungia mishahara kinyume na sheria ya Utumishi wa Umma- Ushaidi upo.
  • Kutumia ofisi vibaya kwakujilipa posho bila kufanya kazi – Safari za mara kwa mara – kwenda Handeni ,Dodoma na Dar-es-saalam, safari binafsi kwa gharama za serikali.
  • Kuwanyanyasa na kuwakandamiza watumishi walio katika idara ya Elimu kwa kuwatishia kuwaondoa pale ofisini.
  • Kutumia Walimu Wakuu ambao ni Wanawake zake kuwaonea na kuwakandamiza walimu waliopo chini.
  • Kuwanyima walimu ruhusa wakati ni haki ya kimsingi na kuwahamisha baadhi ya walimu kwa mchongo apate pesa, wanagawana fedha ya uhamisho na wanaohamishwa.unakuta mwalimu mmoja anahama hata mara tano kwa muda mfupi. Mfano Mwl Hando.
  • Haelewani na wakuu wengine wa idara kutokana na tabia zake hizo mbaya katika Manispaa ya Moshi.
  • Kuficha Maovu wanayofanya wazazi kwa Mabinti zao,wapo watoto wa kike wanalawitiwa na wapo watoto wa kiume wanaonajisiwa lakini kesi zikipelekwa kwa Afisa Elimu anazizima kwa kuchukua rushwa kwa wazazi hao ushahidi upo..
  • Kuna wanafunzi wa shule za msingi wakipata mimba wanashawishiwa watoe ili kulinda nafasi yake hataki ijulikane uchafu uliopo Manispaa ya Moshi Idara ya Elimu..walimu tunaumia sana kuona kizazi kinaharibiwa eti tu kisa kuhofiwa cheo chake kuchafuka..Hafai mtu huyu, uchunguzi ufanyike yatabainika maovu haya..
Mimi ni mtumishi wa Mungu kwani ningekaa kimya wakati naona yanayotokea ni kujitengenezea dhambi mwenyewe.

Mungu atende miujiza kunusuru Manispaa ya Moshi Idara ya Elimu Kwa haya Maovu.

Walimu tunaunga mkono juhudi za Mama yetu Samia Suluhu Hassan na ofisi yako kwa ujumla
Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi ni mpumbavu sana.
 
Kwanini asiupeleke polisi? hapo kuna DAS, DC, RAS na RC kweli hawa wote wanaweza kumshindwa Afisa Elimu? RAS ana mamlaka ya kumhamisha mtumishi yoyote ndani ya Mkoa, kweli anaweza akafanya maovu yote haya bila wao kujua? siamini hata kidogo
Ikiwa shughuli zako hazikupi mwingiliano wa moja kwa moja kama alivuo mtoa mada huwezi kuelewa au kuona, hayo mambo ya hivyo yanafanyika sana. Unashauri mleta mada apeleke ushahidi polisi, uko serious! Hayo ya kulawiti/ kunajisi watoto siwezi kuyaongelea, lakini yanayohusu uhamisho wa mara kwa mara kwa watu walewale, halmashauri ileile kawaida, kugawana/ kuombwa posho hilo linafanywa, unaweza sema ni utashi wa mtoaji ila linawekewa ground. Hilo la kuwa na mahusiano na watumishi wa kike kwa lengo la kuwapa vyeo kawaida, kama unamkeo huku ni mwalimu mkuu, mkuu wa shule, mratibu elimu kata, bro, you are at risk, uniamini usiniamini utajua mwenyewe, huku chini hali iko hivyo. Hivyo sishangai aliyosema mleta mada.
 
Mwenyezi Mungu akulinde na akupe wepesi na umri mrefu ili uendelee kuwa mwakilishi wake duniani. Nami pia naungana na wewe kwa taarifa yako yenye kuakisi maovu mengi ya kweli ambayo walimu wanakutana nayo kazini na maovu hayo yote yapo na yanatendeka kimfumo katika ngazi mbalimbali za kiungozi.

Kwa nini kimfumo? Utakuta viongozi wa walimu ni watu waliofanya kazi sehemu moja kwa muda mrefu na kujenga mazoea kati yao, jambo ambalo linahamasisha upigaji kati yao.

Kiukweli mateso kwa walimu ni mengi sana na hasa walimu wanaofanya kazi vijijini shida ni kubwa na baadhi ya viongozi wanachukulia sehemu za vijijini kama fursa ya utakatishaji wa fedha za umma. Sasa mambo kama haya hayapaswi kufumbiwa macho. Kwa mfano, sehemu nyingi za mijini pesa za nauli za likizo ulipwa mapema lakini kwa halmashauri baadhi za vijijini pesa hizo zinaweza kuchukua hata miaka minne au kulipwa kwa baadhi ya watu ambao utawala unawatambua kimfumo.

Hali kama hizi zinakatisha tamaa na kumpunguzia mwalimu hali kiutendaji. Lakni napenda pia kuipongeza serekali kwa kuleta mfumo wa ESS na mingineyo ambayo inakwenda kupunguza hali hii. Japo kuwa viongozi wenyewe bado kiutendaji hawataki kuendana na mifumo kwa sababu za maslahi yao binafsi. Kimsingi naiomba serekali iongeze mbinyo ili viongozi watumie mifumo katika kufanya kazi na kutatua kero za wananchi.

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Ki ujumla, huku Kilimanjaro kuna ujinga mwingi sana. Division ya elimu na Afya wasimamizi wake ni watu wa hovyo sana. Kuna madudu mengi sana huku.
 
Ikiwa shughuli zako hazikupi mwingiliano wa moja kwa moja kama alivuo mtoa mada huwezi kuelewa au kuona, hayo mambo ya hivyo yanafanyika sana. Unashauri mleta mada apeleke ushahidi polisi, uko serious! Hayo ya kulawiti/ kunajisi watoto siwezi kuyaongelea, lakini yanayohusu uhamisho wa mara kwa mara kwa watu walewale, halmashauri ileile kawaida, kugawana/ kuombwa posho hilo linafanywa, unaweza sema ni utashi wa mtoaji ila linawekewa ground. Hilo la kuwa na mahusiano na watumishi wa kike kwa lengo la kuwapa vyeo kawaida, kama unamkeo huku ni mwalimu mkuu, mkuu wa shule, mratibu elimu kata, bro, you are at risk, uniamini usiniamini utajua mwenyewe, huku chini hali iko hivyo. Hivyo sishangai aliyosema mleta mada.
Point yangu hujaiewelewa mkuu
 
Huyu jamaa ni mkorofi sana sijui huwa anajiamini kitu haishi vizuri hata na wanaomzunguka hata sasa huko Handeni ana mitifuano mikali na jirani yake.
Inasemekana jamaa ameamua kujenga ukuta kwenye eneo la barabarani ili kumzuia jirani yake aside na sehemu ya kupita kuingia kwake. Jirani yake ambaye inasemekana ni Mwalimu katika Halmashauri ya Mji Handeni jina tunalihifadhi kwa sasa lakini jitihada za kumtafuta mwalimu huyo zimeendelea ingawa hata alipotafutwa alisema hayuko tayari kulizungumzia hilo suala.
Ila huyu jama ni kichomi vibaya hawezi kuishi vizuri na wanaomzunguka.
Kila mahali alipoishi siku ya kuondoka kwake ni nderemo na vifijo.
Chanzo chetu cha taarifa kinaendelea kufuatilia suala hili ambalo linahatarisha amani eneo hilo.
Chanzo chetu pia hakikuishia hapo kilijaribu kuwadodosa mafundi ambao wamepewa kazi ya kujenga eneo hilo wamekiri kuwa wao wanafanya tu kama kazi ila pia wanashindwa kuelewa inawezekanaje kwa mtu muelewa kujenga barabarani.
 
Back
Top Bottom