KERO Uonevu unaofanywa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Serengeti

KERO Uonevu unaofanywa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Serengeti

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mganga mkuu wa wilaya anaharibu idara ya afya na kamati ya afya mkoa wanafahamu. Mkurugenzi anafahamu.

Anawasimamisha kazi watumishi bila kufuata utaratibu na bila mkurugenzi kujua. Amewasimamisha watumishi wa kituo cha afya Natta bila Mkurugenzi kushirikishwa (ambaye ni mwajiri).

Amemchukua rafiki yake (anaitwa Mwinuka, ni muuguzi) ndo amemuweka kuwa Katibu wa Afya kinyume na taratibu na katibu yupo amewekwa Nyerere DDH.

Unamuondoa Katibu, unaweka muuguzi ili kupitisha mambo yako. Hata juzi kwenye kikao Rorya kamati ya afya mkoa waliongelea hili.

Huyu Mwinuka ni muuguzi kwanini asiwekwe katibu ambaye ni taaluma yake.

Watumishi wa afya Serengeti tuna mateso, mamlaka zitusaidie
 
Baada ya malalamiko ya mganga mkuu wilaya ya serengeti , Dmo wa serengeti Dr Lusubilo Adam alihamishwa kwenda Dodoma wilaya ya kongwa na Dr chacha alihamishwa kutoka Misungwi kuja serengeti akafika akariport DED madeni hakumpa ushirikiano akaenda Kwa RAS Mara naye hakumpa ushirikiano maana yake kuna coordinated communication baina ya DMO lusubilo na DED wake na RAS Mara

Wizara ikampanga Dr chacha akiyetoka Misungwi kwenda Geita vijijin

DMO wa Geita wizara ikampanga aende Serengeti DED serengeti kampokea Daktari aliyetoka Geita ila Dr. Lusubilo amegoma kukabidhi ofisi na wala Toka apewe uhamisho kwenda Kongwa hajawahi kwenda kuriport maana yake Dr Lusubilo Yuko Juu ya wizara Kwa nini anafanya anachotaka maana yake wizara iko mikononi mwake anafanya anachotaka?
Yeye anang'ang'ania kubaki ili kuendeleza madili yao?? Kama cheo ni kile kile ila mahali kwingine unawezaje kukataa kuhama? Inamaana ananufaika na hapa kwetu Serengeti?
Wizara na Tamisemi tuondoleeni huyu mtu mbona mnatuweka tukose imani kwenu
Kuna harufu ya rushwa kutoka Kwa lusubilo kwenda Kwa DED na RAS kama wao ndio hawataki ahame na hizo hela za kuwahonga anazitoa wapi kama sio fedha za Zahanati mpya zinazowekewa fedha na hazitoi huduma bado?
 
Back
Top Bottom