KERO Uonevu wa wanaokamata Wrong Parking

KERO Uonevu wa wanaokamata Wrong Parking

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Ngurukia

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2023
Posts
4,407
Reaction score
16,942
Kuna jopo la watu limezagaa Dar es Salaam wanaovaa uniform za shati jeupe na suruali nyeusi wanaokamata magari kwa madai ya wrong parking.

Natumia neno kwa madai kwa sababu ni kama wanaotengeza mazingira ya kukamata magari kwa nia ya kutaka kujipatia fedha.

Haijalishi umekidhi vigezo vyote vya kusimama sehemu wanaichukulia ni wrong parking, kama vile kuwasha double hazard, kutokuzima gari, kutozuia magari mengine kupita na dereva kutotoka kwenye usukani.
Bado watakuvamia kama majambazi na kukuzulia kesi.

Huwa wanatembea kwa magroup, jambo la kwanza wanalo force ni kuingia ndani ya gari walilokamata. Hii kiueledi na kiusalama sio sawa. Mbaya zaidi huwa wana kauli mbovu mno zilizojaa vitisho.

Kudhihirisha kuwa kuna kitu hakipo sawa, daima wanakwambia kuwa mtandao una matatizo hivyo hakuna control number ulipe cash tu na kufuata risiti baadae.

Nadhani ifike mahali mamlaka husika ziajiri watu wanaofaa kufanya baadhi ya kazi kuliko kutumia vibaka ambao nia yao ni moja tu kupeleka kila gari yard yao ili kujipatia pesa za commission.
 
Mnawachekea. Kuna siku walinikatamata pale parking ya IFM wanadai wrong parking nawauliza alama ya wrong parking ipo wapi hawana majibu. Wakadai twende ofisin kwao.

1. Nikawadai vitambulisho nikaipiga picha kuichek vizuri nakuta kumbe imesha-expire nikashare kwenye group letu na wanasheria. Wanasheria wakasema hakikisha unakusanya ushahidi wa kutosha hela ya bure hiyo.

2. Nikakubali twende ofisin kwao Ila wasipande gari yangu. Nikampa dogo niliyekuwa nae 50,000 akanunue bidhaa arudi home maana nilijiandaa kumaliza siku Nzima na hao jamaa wa wrong parking.

3. Kufika ofsin wananitisha kuwa faini ni laki 3 na niipeleke gari ndani. Nikapaki nje kibabe. Nikamuambia nionyeshe Ofisi ya boss wako.

4. Kufika ofisin huyo boya akaitwa namuambia anionyeshe kibao kinachokataza kupaki pale anajing'ata ng'ata tu. Boss akaanza kuomba msamaha.

5. Nikachukua details za boss (picha za Kitambulisho na Ile invoice ya kwenda kulipia faini) nikaenda kufungua kesi ya KUJIPATIA MALI KWA UDANGANYIFU nimewaachia wanasheria wanawanyoosha mwaka wa pili Sasa.
 
Mwaka juzi hio Magufuli terminal, tumeenda mdrop dogo adake usafiri aende Kusini, tukaamua tupark pale nje mkono wa kulia ukiwa unatazamia Kimara, siwakaja Sie tukiwa ndani wakaweka machuma yao na kuacha namba ya simu.

Tumerudi tunakutana na hio dhahama, wale wapiga debe wakasema kama kuna nyundo tulivunje tuondoke nalo, nyundo ikawa shida, tukawapigia wakawa wanadelay kuja.

Wamekuja pale wanataka watupigishe fine tukakomaa na dogo, tukasema hii gari haiendi popote, akapigiwa simu mkubwa wao nasie tukampigia simu bro wetu mmoja ni mkubwa mjini pale ,wote wakaja wakabishana pale.

Sijui waliongea nini tukaingia kwenye gari na mmoja wao, tukaenda mbele kidogo tukamshusha tukampa 20k akasepa zake.

Ila bro alisema kama angekataa kupokea ile hela angempeleka hadi nyumbani kwake angejua ye anarudije kwake.
 
Mnawachekea. Kuna siku walinikatamata pale parking ya IFM wanadai wrong parking nawauliza alama ya wrong parking ipo wapi hawana majibu. Wakadai twende ofisin kwao....
Kuna jamaa walimkamata na gari ya kampuni kizembe zembe hivyo na wakaingia kwenye gari yake kwa nguvu. Jamaa hakuwa na story akaendelea na safari yake mpaka ofisni kwao na wakamataji wakiwa ndani.

Kufika ndani ya ofisi wakaanza kushangaa shangaa wakaondoka. Jana sasa wakakutana na jamaa tena katikati ya barabara na kuifunga cheni kwa madai aliwakimbia na gari wameipeleka yard yao.

Ninachojiuliza wanamamlaka gani ya kumtuhumu na kumkata mtu kwa kesi ambayo haijulikani kisheria?
 
Ukiachana na uhalali au uharamu wa hao maofisa kukamata magari kwa wrong parking, kwa jiji la Dar es Salaam kukamata magari kwa wrong ni lisilo na maana yoyote au haramu kutoka Mwanzo.

Ili ulifanye liwe halali, ni lazima uwe umetenga maeneo maalum kwa ajili ya maegesho ya magari, sasa je Serikali ina maeneo ya umma ya kuegesha magari?? Kama hakuna, unataka watu wakapaki magari wapi wanapokuja nayo mjini, kama sio pembeni mwa barabara wanazotumia kufika mjini?

Bila kuweka maegesho, kukamata magari kwa jina la wrong parking ni uonevu, ni haramu.
 
Tatizo ni kuwa TARURA wametoa kandarasi kwa kampuni binafsi kukamata magari kwa makubaliano ya commission kwa kila gari linalokamatwa na kufikishwa yard.

Na hiyo kampuni nao imeajiri vijana wa ovyo kukamata magari kwa ahadi kila group litakalokamata gari na kuweza kulipishwa fine basi wanapewa fungu la commission.

Sasa kinachotokea hapa ni kama fungulia mbwa, kila mtu anavutia upande wake ili apate commission.

Hakuna tena wrong parking bali ni matakwa ya group la panya road (nawamithilisha na panya road maana ni vijana wahuni wa hovyo kabisa) litakalokukamata kuamua kukupa kesi ya wrong parking.
 
Kuna jamaa walimkata na gari ya kampuni kizembe zembe hivyo na wakaingia kwenye gari yake kwa nguvu. Jamaa hakuwa na story akaendelea na safari yake mpaka ofisni kwao na wakamataji wakiwa ndani.

Kufika ndani ya ofisi wakaanza kushangaa shangaa wakaondoka. Jana sasa wakakutana na jamaa tena katikati ya barabara na kuifunga cheni kwa madai aliwakimbia na gari wameipeleka yard yao.

Ninachojiuliza wanamamlaka gani ya kumtuhumu na kumkata mtu kwa kesi ambayo haijulikani kisheria?
Hao jamaa tatizo hawajawahi pigwa, siku wakikutana na kipigo hakika wataheshimu watu
 
Hawa wa dar ni CHANGAMOTO na ni vibaka maana wanapalamia gari huku unaongea huku wanafungua milango wanaingia kwenye gari hzo ni dharau
jamaa ni vibaka tu. Nina hakika wakiingia kwenye gari na kuona simu imekaa kizembe wanapita nayo.
 
Back
Top Bottom