Uongo huaminika sana

Uongo huaminika sana

Kuna jamaa kamuuliza mwenzie hapa.
Hapa nyumbani umeshindwa kule kwao utaweza?
 
Wakati wa usajiri siasa uongo na kiki kwa viongozi wa timu za mpira hutamalaki.

1. Wakati wa uchaguzi wa kumchagua Rais wa timu hiyo kuna mchezaji alitumika kama kiki ili Rais achaguliwe kwa kishindo. Nilimsikia akisema nimeleta high profile player kutoka Ligi Kuu ya Uingereza timu ya Newcastle UTD, nilicheka sana.

2. Kuna mchezaji alitambulishwa usiku wa manane huku watambulishaji wakijinadi huyu ni kwa ajili ya mechi za kimataifa, nilicheka sana.

3. Mwishon wa usajiri akasajiliwa mchezaji anasifika kwa kukimbia, wachambuzi wakapanga kikosi wakasema kule M huku T master kati dokta juu kidogo Key aise hamna wakutuzuia kimataifa, nilicheka sana.

4. Wakaletwa vijana wawili kama waongeaji wa timu hiyo mmoja ni Mkuu wa mambo ya Digitali, mmoja wao akasema tunaenda makundi maana timu tutayokutana nayo round ya kwanza haina kikosi, inajitafuta tu. Kingine sasa hivi sisi ni wakubwa hapa Africa Mashiriki, nilicheka sana.

5. Sasa hivi kuna wimbo wanasema lazima makundi hii timu itaenda maana wana kikosi bora sana kuliko timu yoyote Africa mashariki, ngoja tuone.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Hivi PSG, Man city waseme nini ? Katika msimu mmoja tu Yanga unataka iwe kama Al Ahly?
 
Takwimu zinaongea, Tafuta timuyako yoyote unayo iamini kuwa yenyewe ni Bora apa Tanzania kuliko Yanga alafu linganisha izo takwimu.
Huitaji kubishana na mtu, fanya tathmini na atuhitaji jibu sisi majibu tunayo ila jiridhishe wewe mwenyewe.
Jamaa anaongelea kimataifa wewe uko kitaifa

Sent from my LM-Q730 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom